MAINDA AMRUDIA MUNGU KWA KUACHA KUVAA VIMINI

IMEKAA poa sana! Shosti anayesukuma maisha kupitia mgongo wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameahidi kufanya mabadiliko ya mavazi kuanzia kwenye filamu hadi maisha yake binafsi.
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mainda alisema kuanzia sasa watu wategemee mabadiliko makubwa katika maisha yake kwani ameamua kuvikacha viminihivyo anaishi katika matakwa dini.
“Nitafanya filamu za kumtukuza Mungu hata kama zitakuwa si za kumtukuza moja kwa moja ila zitakuwa na maadili mazuri yasiyopotosha jamii na kumuudhi Mungu, sitavaa vimini tena,’’ alisema Mainda.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger