Showing posts with label MAINDA. Show all posts
Showing posts with label MAINDA. Show all posts

MAINDA: "SIMWANIKI MUME MTARAJIWA, ILI WAJANJA WASIJE KUMUIBA KAMA WALVYONIIBIA RAY WANGU"

STAA wa filamu Bongo ambaye amejikita kumtumikia Bwana kwenye wokovu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kamwe hawezi kuainisha sifa za mwanaume anayehitaji aolewe naye kama ilivyo kwa mastaa wengine kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema japo umri wake unaruhusu kuolewa hawezi kuweka wazi sifa za mwanaume anayehitaji awe wake kwa kuwa huenda sifa anazozihitaji Mungu hajampangia kuolewa na mtu wa aina hiyo.
“Kwenye maono naona kabisa mume wangu yupo karibu ambaye Mungu ameniandikia, sasa siwezi kusema nahitaji mwanaume mwenye sifa zipi sababu nikisema nahitaji awe hivi kumbe Mungu hajanipangia huyo,” alisema Mainda.
Read more >>

SASA PENZI LA MAINDA LAGOMBEWA KAMA PIPI..NI SHIDAAAA

Staa  wa  Filamu  za  Kibongo  aliyeamua  kumpokea  Yesu, Ruth Suka  'Mainda'  amesema  amekuwa  akipata  wakati  mgumu  kumjua  mwanaume  wa  kweli  ni  yupi  ambaye  anaweza  kumuoa  na  ndoa  yake  ikawa  na  raha  badala  ya  majuto  kama  ilivyo  kwa  baadhi  ya  wasanii  wenzake....

Mainda  alisema  hakuna  kipindi  kigumu  kama  kujua  yupi  ni  mwanaume  sahihi  wa  kumuoa  na  hili  limekuwa  likiutesa  moyo  wake  japo  sasa  ameamua  kumwachia Mungu  wake  ili  amsaidie  kwani  kwa  akili  zake  ameshindwa...

"Hakuna  wakati  mgumu  kama  kipindi  cha  kumpata  mume  sahihi  kutoka  kwa  mungu, kwani  ukijichanganya  unaweza  kuchukua  mwanaume  ambaye  si  wako  na  kusababisha  kuwe  na  mafarakano  ndani  ya  ndoa  na  hili  ndio  linaumiza  kichwa  changu  kwani  mpaka  sasa  sijajua  ni  yupi  kati  ya  wengi  wanaohitaji  kunioa," alisema  Mainda

Msanii  huyo  alisema  anajifunza  mambo  mengi  kupitia  ndoa  za  watu  waliomtangulia  kwani  nyingi  zimejaa  vurugu  likiwemo  suala  la  kusalitiana  na  kuambukizana  magonjwa  ya  zinaa  kama  vile  Ukimwi  na  menginenyo, hivyo  naye  hatapenda  awe  miongoni  mwa  ndoa  hizo
Read more >>

MAINDA AWAJIBU WANAOHOJI ULOKOLE WAKE, UKWELI WOTE UPO HAPA

Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’  amefunguka kuwa kwa sasa hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya wokovu.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa jicho lingine wanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda.
Read more >>

MAINDA AMRUDIA MUNGU KWA KUACHA KUVAA VIMINI

IMEKAA poa sana! Shosti anayesukuma maisha kupitia mgongo wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameahidi kufanya mabadiliko ya mavazi kuanzia kwenye filamu hadi maisha yake binafsi.
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mainda alisema kuanzia sasa watu wategemee mabadiliko makubwa katika maisha yake kwani ameamua kuvikacha viminihivyo anaishi katika matakwa dini.
“Nitafanya filamu za kumtukuza Mungu hata kama zitakuwa si za kumtukuza moja kwa moja ila zitakuwa na maadili mazuri yasiyopotosha jamii na kumuudhi Mungu, sitavaa vimini tena,’’ alisema Mainda.
Read more >>

BAADA YA KUTOSWA NA RAY MAINDA SASA ATANGAZA KUSAKA MUME

STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kwa sasa hahitaji mchumba wala mpenzi, anahitaji mume wa kumuweka ndani.
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema hata akifuatwa na mtu mwenye fedha nyingi kutaka uhusiano naye, hawezi kumkubalia kwani anachotaka sasa hivi ni ndoa tu.
“Kwa sasa mpenzi wangu ni Yesu na kutokana na yeye mume wangu nimeshamuona kwenye maono…yulee anapiga hodi sura yake,” alisema Mainda.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger