Uhalisia
wa ajali iliyotokea Jumamosi (Juni 21, 2014) na kusababisha vifo vya
watu sita na wengine 16 kujeruhiwa vibaya maeneo ya Lugalo.
Ajali hiyo ilitokea juzi Jumamosi (Juni 21, 2014) ambapo kwa mujibu
wa mashuhuda, chanzo kimetajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa daladala
iliyokuwa ikitokea Tegeta kwenda Mwenge ambayo ilichepuka na kuingia
katika ‘saiti’ ya wanaokwenda Tegeta, ikaigonga ubavuni daladala
nyingine iliyokuwa ikielekea Tegeta.
Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
“Dereva wa Coaster lililotokea Tegeta
alikuwa spidi kuelekea Mwenge, alipoona kuna foleni katika upande wake,
akachepuka ghafla kwenye maungio ya barabara na kulivaa ubavuni Coaster
lililokuwa likielekea Tegeta,” alisema shuhuda huyo.
HAYA NDIO MAPICHA BIRTHDAY YA DIAMOND ILIVYOKUWA, TAZAMA KITANDA ALICHOANDALIWA KUJIACHIA NA WEMA NA SHIDAA
Madereva wa magari yote mawili walidaiwa kutoweka kusikojulikana muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea huku baadhi ya miili pamoja na majeruhi hao wakipelekwa katika Hospitali ya Lugalo.
No comments:
Post a Comment