Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yake.
VITUKO uswahilini! Mtoto wa mwenye umri umri wa mwaka mmoja ambaye
jina halikufahamika ameokolewa na Oparesheni Fichua Maovu ya Global
Publishers baada ya kudaiwa kutelekezwa kwa siku nzima na mama yake
mzazi, Mama Sofia.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Juni wikiendi iliyopita maeneo ya
Somanga-Magomeni, Dar ambapo kwa mujibu wa wasamaria wema waliomuona
mtoto huyo, alionekana majira ya asubuhi akirandaranda barabarani.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Mtoto huyo akiwa na msamaria.
Baadaye OFM ilipewa taarifa na kufika eneo la tukio ambapo ilipata
maelezo kuwa mama wa mtoto huyo huwa na tabia ya kumwacha mwanaye mara
kwa mara mtaani bila kumjali.
OFM ilifikisha suala hilo kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye alimtambua mtoto huyo mara moja kwa kuwa alikuwa akiishi naye nyumba moja hivyo alimpeleka kwa wazazi wake huku akiwapa onyo kali.
No comments:
Post a Comment