MWENYEKITI wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),
Simon Mwakifwamba amefunguka kuwa kinachowaponza wasanii wa filamu Bongo
kiasi cha kuwa ombaomba ni kupenda starehe.
Akichonga mbilitatu na paparazi wetu, Rais huyo alisema wasanii
wamekuwa watu wa kupenda sana kupiga mitungi na kufanya starehe nyingine
kwa kutumia fedha nyingi kitu kinachowapelekea kutokuwa na maendeleo
katika maisha yao na kuishia kupiga mizinga tu.
“Wasanii wanapata fedha lakini cha kushangaza wanashindwa hata
kujiunga na bima za afya au kuwekeza kwenye mambo muhimu, yaani mtu
kutoa kiwango fulani cha fedha kwa ajili ya maisha yake ya baadaye
anaona kama atamaliza fedha zake,” alisema Mwakifwamba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment