MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula
‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi
kikubwa wasanii wamebadilika kitabia.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa
duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau
na kuponda raha mfululizo.
“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na
kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia
Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment