Showing posts with label JOHARI. Show all posts
Showing posts with label JOHARI. Show all posts

JOHARI AZIDI KUTESEKA PENZI LA RAY, AMWAMBIA IPO SIKU ATAMRUDIA TU, SOMA ALIYOFUNGUKA JOHARI HAPA

MKONGWE katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuendelea kuteseka na penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ baada ya kunaswa akimzungumzia.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Viwanja vya Leaders Club kwenye uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo Johari alikuwa amekaa na kruu yake (huku  wakigonga ulabu) ndipo mmoja kati wenzake hao, akagusia stori za Ray kisha Johari alicheka na kusema ipo siku Ray atarejea katika mikono yake.
Mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Ipo siku ambayo haijulikani tarehe wala mwaka Ray lazima atarudi katika mikono yangu kwani namfahamu sana Ray kuwa ni mtu wa kuruka lakini kwangu amefika,” alisikika Johari.
Read more >>

JOHARI: BAADA YA RAY KUNITOSA, KWA SASA BADO NIPO NIPO SANA

MKONGWE kwenye kilinge cha sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amewataka mashabiki wake wajue kwamba, muda ukifika wa kupata mume wa kufunga naye ndoa, atafanya hivyo lakini kwa sasa anatoa kipaumbele kwenye kazi tu.
Mkongwe kwenye kilinge cha sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na Amani, Johari ambaye umri wake upo juu ya miaka 30, alisema watu wengi wanafikiri kuwa ndoa ndiyo kila kitu katika maisha lakini kwa upande wake bado hajaifikiria.
“Kitu ambacho nakiamini mimi ni kwamba ndoa kama nimepangiwa na Mungu ipo na itaendelea kuwepo haijalishi hata kama nitafikisha miaka hamsini,” alisema  Johari.
Read more >>

JOHARI AMCHANA IRENE UWOYA, PIA AWACHANA WAIGIZAJI WA KIKE WANAOJICHIA NA KUPOTEZA MVUTO

Msanii  Johari Blandina ‘Chagula’ ambaye ni star mkongwe Swahiliwood amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuutunza muonekanio wake na kuwa kama kijana licha ya umri wake kuwa mkubwa tofauti na baadhi ya waigizaji wenzake wa kike ambao hujiachia na kuonekana wazee licha ya umri wao kuwa mdogo.

Akizungumza na Filamucentral Johari alisema:

“Wasanii wa kike wengi ni watoto wadogo lakini kwa sababu ya kujiachia wanaonekana kama watu wazima lakini ukweli ni watoto wadogo sana, namshukru Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini mwili wangu upo fiti,”
 
Johari alimtolea mfano Irene Uwoya ambaye ni shoga’ke wa karibu kuwa anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya kujiachia licha ya kwamba amempita miaka kadhaa. 
johari
 
Vile vile Johari amesema kuwa kawasasa amerudi kwa moto wa kasi kama muigizaji kama awali baada ya kuwa upande wa producer kuwapa nafasi chipukizi ambao wengi amesema wameshindwa, hivyo amerudi mwenyewe kwenye game.
Read more >>

JOHARI AKANA KATUKATU MADAI YA KUBATIZWA

MKONGWE wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amedaiwa kubatizwa juzikati katika Kanisa Katoliki Nyalikungu wilayani Maswa, Simiyu lakini mwenyewe amekanusha.
Mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Chanzo makini kilichodai kushuhudia ubatizo, kilieleza kuwa Johari alifika Jumapili kanisani hapo na watu kuhoji kwa nini achelewe kubatizwa? Alipotafutwa na mwanahabari wetu, Johari alitiririka:
“Kweli nilikwenda kwenye hilo kanisa lakini sikubatizwa kama alivyosema huyo mtu. Nitabatizwaje mara mbili? Mimi nilishabatizwa tangu utotoni.”
Read more >>

RAY ASHINDWA KUMZIKA BAM’DOGO WA JOHARI, KISA KIZIMA SOMA HAPA

MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.
Mkurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’
Mzee huyo alifariki katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya presha na figo yaliyokuwa yakimsumbua na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali wa filamu nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
 Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula akiwa msibani.
Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema:
“Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini,” alisema Ray.
Read more >>

MASIKINI, JOHARI AFIWA NA BABA YAKE MDOGO


Msanii Blandina Chagula 'Johari' baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la baba yake mdogo Mzee Clement Chagula.
Baadhi ya mastaa wa Bongo Muvi walioshiriki mazishi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii Steve Nyerere (kulia) na Mrisho Mpoto 'Mjomba'.
Mastaa wa Bongo Muvi wakiwa na Johari.
Kaburi la baba mdogo wa Johari, Mzee Clement Kiyenze Chagula.
STAA wa Bongo Muvi, Blandina Chagula 'Johari' amefiwa na baba yake mdogo Mzee Clement Kiyenze Chagula aliyezikwa leo. Marehemu Chagula amefariki akiwa na miaka 63. Mazishi hayo yalihudhuriwa na mastaa kibao wa filamu nchini akiwemo Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete.
Read more >>

MFUNGO WAMBADILI JOHARI KWA KUFAA MAVAZI YA KIHESHIMA, MUONE HAPA

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema amewaunga mkono Waislamu kwa kuvaa mavazi ya kujistiri na kuziba sehemu kubwa ya mwili kuheshimu mwezi wa Ramadhani.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Johari alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu dini zote ni za Mungu na kwa kuwa ni kipindi cha Ramadhani, amebadilika kwa kila kitu.
“Kipindi hiki ni cha kumrudia Mungu, nimeacha kila kitu kibaya kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na nimeamua kutulia ili nipate muda mwingi wa kuomba,” alisema Johari.
Read more >>

WASANII WAMCHEKA JOHARI WA BONGO MOVIE

 Msanii mkongwe wa filamu Bongo Blandina Chagula ‘Johari’
WASANII wa filamu Bongo, waliokuwa katika kamati maalum iliyoundwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ya kukabidhiwa ukamanda wa vijana, juzi walimcheka mwenzao, Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kunyang’anywa bwana.

 Tukio hilo lilitokea juzi maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo wenzake walimcheka kutokana na aliyekuwa mpenziwe, Vicent Kigosi ‘Ray’ kuporwa na mwigizaji mwenzake, Chuchu Hans.
 “Niachieni Johari wangu jamani, mnamkerakera kila wakati hadi anakosa amani kwani wanaume wameisha atapata mwingine” alisikika Steve Nyerere akimfariji msanii huyo mkongwe ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray.
Read more >>

MASHABIKI WALILIA PENZI LA RAY, JOHARI, HAWAMTAKI CHUCHU, SOMA HAPA

MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
Mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.
Read more >>

JOHARI AWANYAMBA WAIGIZAJI WANAOKATISHWA VIUNO MBELE YA HADHARA.



Blandina  Chagula  'Johari'  ambaye  ni  mmoja  wa  washiriki  wa  filamu  mpya  ya  Wrong  Hope  amewaponda  wasanii  wa  filamu  wanaokubali  kukatishwa  viuno  mbele  ya  hadhara  na  kueleza  kwamba  kamwe  kwa  upande  wake  hawezi  kufanya  jambo  hilo  hata  kwa  malipo  namna  gani...!!!

"Siwezi  kujidhalilisha  mbele  ya  umati  kwa  kukata  kiuno, ni  ulimbukeni  tu kukata  viuno  mbele  ya  watu, labda  niwe  nimelewa  kiasi  cha  kutojitambua  ndo naweza  kufanya  madudu  kama  hayo," alisema  Johari.
Aidha, Johari  alisema  kuwa  kuna  umuhimu  kwa  wasanii  wa  filamu  kujitambua  na  kufanya  mambo  ya  maana  kwa  jamii  kuliko  kujigeuza  kituko  na  kufanya  mambo  ya  ajabu.

Mrembo  huyo  alihitimisha  kwa  kuwaomba  mashabiki  wake  waipokee  kwa  mikono  miwili  filamu  yake  mpya  ya  Wrong  Hope  itakayotoka  mwezi  ujao  ambapo  ndani  yake  yumo  Mohammed  Nurdin  'Chekbudi'  na  marehemu  Sheila  Haule  'Recho'.
Read more >>

JOHARI: WASANII WENZETU KUFARIKI, IMEKUWA FUNDISHO KWETU

MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii wamebadilika kitabia.
Mkongwe kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau na kuponda raha mfululizo.
“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
Read more >>

JOHARI: NITAMLILIA RECHO MILELE, KWANI NAMKUMBUKA KWA MENGI SANA

STAA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kifo cha msanii mwenzake Rachel Haule ‘Recho’ hakitafutika kichwani mwake kirahisi, kwa kuwa anamkumbuka kwa mengi.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akilia kwa uchungu katika mazishi ya msanii mwenzake katika tasnia ya filamu, Recho Haule.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Sinza – Palestina kulipokuwa na msiba wa Recho, Johari alisema Recho alikuwa na kiu ya kufika mbali na hakuchoka kuomba ushauri na kuufanyia kazi.
Recho haule (kushoto) akiwa na mke wa Mtitu enzi za uhai wake.
“Amefanya kazi na RJ Company muda mrefu, baadaye akaamua kuanza kufanya kazi zake akishirikiana na Saguda. Mwanzo ulikuwa mzuri sana, alikuwa akitaka kitu chake anaweza kupiga simu hadi usiku kuomba ushauri. Kwa kweli sitamsahau, nitamlilia milele,” alisema Johari.
Read more >>

ZIJUE SIFA ZA JOHARI, NA KAMA UNATAKA KUMUOA BASI USILAZE DAM7


Staa mkubwa wa filamu za Kibongo Blandina Changula "Johari"
Makala: Sifael Paul
Julai 28, 1983 mkoani Shinyanga, alizaliwa mtoto wa kike ambaye sasa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Ni maarufu kwa jina

la kistaa la Johari lakini majina yake kamili ni Blandina Changula.
Kama kawaida yetu huwa tunatoa nafasi kwa staa kusimulia alikopitia hadi akafikia mafanikio aliyonayo ili kutoa chansi kwa

Blandina Changula "Johari" akiwa kwenye pozi
wengine kujifunza au kutamani kuwa kama yeye. Yaani kutoka ‘ziro’ hadi ‘hiro’. Leo tunaye Johari kwenye spesho intavyu.
UNGANA NAYE.
Sifael: Johari ni nani?
Johari: Ni staa mkubwa wa Bongo Movies.
Sifael: Elimu yako ni ipi?

Johari: Nimepata elimu yangu ya msingi mkoani Shinyanga katika shule iitwayo Bugoyi.
Nilihitimu mwaka 1996. Baadaye nilipata elimu yangu ya sekondari kwenye shule inayoitwa Buluba kulekule Shinyanga kabla ya

kuja kumalizia elimu yangu kwenye Shule ya Greens ya Dar.
Nilipomaliza kidato cha nne nilisomea mambo ya ‘usekretari’ na baadaye nilisomea mambo ya hoteli hapahapa Dar.

Sifael: Ulianza lini mambo ya kuigiza?
Johari: Nilianza kujiingiza kwenye mambo ya sanaa tangu nikiwa mdogo. Nilianza kuigiza nikiwa shule ya msingi na kanisani.

Nilipenda kuigiza tangu nikiwa mdogo.
Sifael: Ulianza lini kuigiza rasmi?

Johari: Nilianza kuigiza rasmi kupitia Kaole Sanaa Group pale Kigogo, Dar. Nilienda kwa mara ya kwanza kwenye kundi hilo

nikaomba fomu ya kujiunga na kuanza kufanya mazoezi ya kuigiza.
Sifael: Unakumbuka ilikuchukua muda gani wa mazoezi hadi ukaonekana runingani?
Johari: Ilinichukua kama mwaka mzima nikifanya mazoezi na kundi hilo kabla ya kupata nafasi ya kuigiza rasmi kwenye michezo

ya runinga.
Sifael: Ulikuwa na akina nani?
Johari: Nyota yangu ilianza kung’aa nilipokuwa na Steven Kanumba (kwa sasa marehemu) na Vincent Kigosi ‘Ray’ ambao

walinishawishi kuachana na michezo ya runingani na kuanza mchakato wa kufanya filamu.

ITAENDELEA WIKI IJAYO
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger