FRORA MBASHA POLE SANA...
NIJUAVYO
MIMI NI KWAMBA, WAANDISHI WA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI TUNAONGOZWA NA
KANUNI NA SHERIA! NA KAZI KUBWA NI KUIELIMISHA JAMIIBADALA YA
KUKANDAMIZA NA KUPOTOSHA JAMII. KWA
JINSI HIYO NI LAZIMA IFIKE MAHALI TUONE KWAMBA KUMDHALILISHA MTU ,PAMOJA NA KUINGILIA UHURU WA MTU BINAFSI NI MAKOSA!
Kinachoe
delea sasa ivi juu ya Flora&Mbasa ni kwamba tunaingilia maisha
binafsi ya mbasha na mbaya zaidi tunamdhalilisha ''MWANAMKE'' Flora..kwa
sasa tunauza sana magazeti na tunapata trafiki kubwa kwenye blogs zetu
ili kujiingizia kipato..kwa Kumdhalilisha Flora ndicho kinachoendelea...
Kama
tumeamua kuchukua jukumu la Mahakama sawa. Maana ndicho tunachokifanya
kila kona kujaribu kutoa hukumu ya kesi hii! Mbaya zaidi 99%
tunamuhukumu Flora eti kwa misemo kwamba MWANAMKE MPUMBAVU hubomoa
nyumba yake mwenyewe!
Ni lini huu mfumo dume ndani yetu
utaondoka? Kosa linalomkabili mume wa Flora liko wazi wazi, na vitendo
hivyo vinafanyika sana sana ndani ya nyumba zetu. Ni vitendo vya
kumdhalilisha Mwanamke sana na vinatuumiza sana kina mama wengi. Hakuna
mwanamke atakaependa kusikia mumewe kamdhalilisha kwa kulala na mwanamke
mwingine. Tena mdogo wake??! Tena kwa kubaka! Hakunaaaaa! Hayupo huyo
mwanamke...
Nikijaribu kuvaa viatu vya Flora ni vizito sana. Wala sijui ningefanya nini kwa maumivu ninayohisi....
Kinachoniumiza
ni kwamba jamii imeacha HOJA ya msingi ambayo ni kitendo alichofanya
Mbasha na ndicho kimempandisha kizimbani Mbasha!! na badala yake jamii
kuanza kumuona Flora ni mkosefu kuliko aliyebaka..
Kwa maneno
mengine ni kwamba tunabariki alichokifanya mbasha, na kwamba Mwanamke
yeyote asichukue hatua yeyote endapo Mume atabaka au kutoka nje ya Ndoa
yake.
Yaani mnatuambia wanawake wa nchi hii kwamba, ukimfumania
mumeo au akibaka we umsamehe kimya kimya na maisha yaendelee! Mpaka sasa
jamii haioni kwamba Mbasha amefanya kosa kabisa! Kana kwamba kama
Mbasha hatakiwi kukemewa bali asifiwe mwanzo mwisho na zawadi apewe kwa
kitendo hicho kama atakutwa na hatia kwamba amefanya...
yaan
kwenye jamii yetu inaonekana mwanaume kua na mahusiano nje ya nyumba
yake ni Sifa tena anapewa majina mazuri ya urijali! lakini kwa mwanamke
ni umalaya na Ukahaba...
Hapo ndo napataga wazimu wa kichaga
aiseee... Inaniumiza sana na kuna siku nilikaa nikaamua kuvunja ukimya
juu ya hili jambo la michepuko tena nikawataja wazi wazi watu
tunaowategemea wawe mifano bora lakini wao ndo waharibifu wakubwa! Cha
ajabu jamii iliinuka juu yangu ila ukweli ulisimama na unabaki palepale
kwamba mtu anapotoka nje ya Ndoa yake au nyumba yake ni MZINZI na
anatakiwa akemewe bila kuangalia Hadhi yake.
kinachofanyika sasa
kwenye jamii ni UNYANYASAJI DHIDI YA MWANAMKE NA UKATILI WA KIJINSIA
pale tunapowaona wanaume WAzinzi ni marijali na Wanawake ndo Malaya na
makahaba...
mbaya zaidi kuna baadhi ya wanawake wenzetu
wanaushadadia huu MFUMO DUME kiasi kwamba wanakua mstari wa mbele
kumnyooshea Flora vidole huku wakisahau kua mwenzio akinyolewa na ww
zako tia maji..WANAWAKE TUSIMAME IMARA KUTOKOMEZA UKATILI NA MFUMO DUME
kwenye jamii yetu...Kama kuna mwanamke atakaesherehekea mume wake
akimbaka mdogo wake basi huyo amnyooshee kidole Flora...
Nasisitiza! ni kwa nn mwanaume husifiwa kwa uzinzi Na jamii inatetea???! HUU NI MFUMO DUME na ni Ukatili dhidi ya Wanawake...
MIMI
JOYCE KIRIA NASEMA, MAADILI YAZINGATIWE NA WATU WOTE BILA KUJALI
WADHIFA WA MTU. NA ENDAPO MTU AKIKENGEUKA BASI JAMII IMKEMEE VIKALI.
BADALA YA KUTUKUZA UZINZI KWA KUANGALIA STATUS ZA WATU NA KUKANDAMIZA
WANAWAKE....
kwa pamoja tunaweza kutokomeza ukatili huu.....
NOTE: WAKINA MAMA TUPIGE MAGOTI TUMLILIE MUNGU ASEME NA HAWA WATU WANAOTAWALIWA NA PEPO MCHAFU WA UZINZI..IN THE MIGHT NAME JESUS I PRAY....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment