Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa
hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya
wokovu.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata
shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu
wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama
atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza
vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa
jicho lingine wanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya
kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si
mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment