STORI MFUPI YA NILIKUA NA MPENZI, INASISIMUA ISOME HAPA
George
Iron Mosenya Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu
alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea
akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana
naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na
msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika
nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo
wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya
baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi
nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli.
Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli
nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia
chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki
walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno
lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA
MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha
kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja
tu…NGONO… na
katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia
vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa
anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono
ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha
kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi
bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali
zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni
uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na
pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka
kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama.
“Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia
neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye
tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule
kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu
huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni
nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini
ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika
pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine.
Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima
penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana
naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia
kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili
atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya
tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni
ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru
lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida
ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake
madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa
hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo
akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu,
nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake,
kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku
na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze
kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga
namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka
kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa
nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA
AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua
sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo
lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa
haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema,
binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria
wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu.
Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na
kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa
nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na
niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada
ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu.
Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE
baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu
ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa
maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa
mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda
uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa
naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba
yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi
hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji
iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako
haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari
kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi
lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala
usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa
mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake.
Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi
ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu
…nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa
nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi
kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni
heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu
ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama
ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa
kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu,
nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na
mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili
siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta
napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya
kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini
ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani
kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine
dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi
aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau
mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na
hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE
MTUMWA!!!! SHARE KWA WENGINE MWISHO!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment