Showing posts with label NISHA. Show all posts
Showing posts with label NISHA. Show all posts

MASAI NYOTAMBOFU AFUNGUKA KUHUSU KUTOKA KIMAPENZI NA MTOTO MZURI NISHA

 
Mchekeshaji maarufu hapa Tzee ambaye anamiondoko ya kimasai, Gillady Severina aka Masai Nyotambofu, ameteka sana soko la filamu hapa Bongo kwa upande wa Comedy kwa kufanya filamu kibao kama ‘Vyumba Vimejaa’, ‘Inye Ndembendembe’, ‘Pedeshe’ nk.

 
Kwa chanzo chetu cha kuaminika kimebaini uhusiano uliopo baina ya Masai Nyotambofu na Salma Jab aka Nisha anayetamba sokoni na muvi ya ‘Zena Na Betina’, ‘Jike Dume’ nk, mara baada ya kuunasa Comment yake Instagram aliyopost kidume mwenye mbwembwe za kimasai. BK lilijaribu kumuuliza Nyotambofu ambye alijibu hivi...
“No jamani mimi sina mahusiano yeyote na Nisha but mimi siku ile nilipost tu kuwataarifu watu juu ya kutoka kwa muvi yake Nisha iliyofahamika kwa jina ‘Zena Na Betina’ basi najua Nisha alitoa Coment hiyo kwasababu aliona kuwa mimi jinsi gani napenda mafanikio yake.” alisema Masai Nyotambovu.
Read more >>

TETESI ZA NISHA KUJIUNGA NA FREEMASON, SOMA ZAIDI HAPA

STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.
Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.
Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.
Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.
Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.
“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na  kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.
Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.
Read more >>

NISHA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KUHUSU KUWA MJAMZITO...!!!

 
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ 
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amepangua madai kuwa ni mjamzito na kudai ni maneno ya ya watu licha ya kwamba ukikiangalia kwa makini kitumbo chake unaweza kuhisi kuna kitu ndani.

Akizungumzia madai hayo na kwamba ndicho kinachomfanya asijichanganye na wenzake kama kawaida, Nisha alisema kutoonekana kwake ni maamuzi tu. “Eti nina mimba!

Mh…nashangaa sana, sijui watu wanatoa wapi hayo maneno, mimi sina mimba na nilikuwa sionekani kwa sababu nilisafiri, pia mwezi mtukufu huwa sitoki hovyo, nikiamua kuzaa watu wataniona tu,” alisema Nisha.
Read more >>

NISHA: MH! ETI NINA MIMBA, WATU BWANA, WATU KWA UMBEYA

MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amepangua madai kuwa ni mjamzito na kudai ni maneno ya ya watu licha ya kwamba ukikiangalia kwa makini kitumbo chake unaweza kuhisi kuna kitu ndani.
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
Akizungumzia madai hayo na kwamba ndicho kinachomfanya asijichanganye na wenzake kama kawaida, Nisha alisema kutoonekana kwake ni maamuzi tu. “Eti nina mimba! Mh…nashangaa sana, sijui watu wanatoa wapi hayo maneno, mimi sina mimba na nilikuwa sionekani kwa sababu nilisafiri, pia mwezi mtukufu huwa sitoki hovyo, nikiamua kuzaa watu wataniona tu,” alisema Nisha.
Read more >>

NISHA: NIMECHEZEWA SANA NA WANAUME, KWA HIYO SITAWAAMINI TENA KATIKA MASUALA YA KIMAPENZI


Msanii wa Filamu za kibongo Salma Jabu 'Nisha' amedai kuwa hamjui mwanaume atakayeweza kuitwa baba wa watoto wake kwani kila mwanaume anayemtaka kimapenzi huwa haamini kama anaweza kutimiza hilo katika maisha yake ya mapenzi.....
Nisha alisema hivi sasa ni mapema sana kuwa na mawazo ya namna hiyo kwani bado anatafakari, na kudai hawezi kuweka asilimia nyingi wakati bado yeye ni kijana na anatafuta hela kwa sasa na si familia.....

"Nahitaji kuweka akili chini kwa sababu ishu ya kuzaa au kuwa na mwanaume ambaye anaweza kulea watoto si kitu kidogo, ni lazima akili yangu itulie na ifanye maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu vinginevyo naweza kulia kwa sababu sitakuwa na maamuzi sahihi ambayo yatanifanya niishi kwa raha," alisema Nisha.

Muigizaji huyo tangu aanze kupata jina amevurugwa na wanaume kadhaa kimapenzi akiwemo staa wa bongo fleva Ney wa Mitego, ambaye uhusiano wao ulionekana kama wa kutaka kiki kabla ya kutemana ghafla
Read more >>

DONGO: NISHA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KUHUSU KASHFA YA KUTUMIA JUJU.

Mwanadada kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
MWANADADA kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amewabwatukia wasanii wenzake wanaomshutumu kwamba anatumia ndumba na kuwataka waache maneno hayo.

Nisha aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kuzagaa kwa tetesi kuwa alizomewa na wasanii wenzake wakimwita mchawi kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa haraka kwenye sanaa, tofauti na wasanii wengine wanaosota kwa muda mrefu mpaka kupata mafanikio. 
“Unajua siku zote mti wenye matunda ndiyo huwa unapigwa mawe, kipindi nikiwa bado sijaweza kucheza filamu zangu, yaani nikiwa chipukizi hakuna aliyekuwa ananizungumzia lakini sasa hivi wananiongelea kila kona, anayesema mimi ni mchawi basi huwa tunawanga pamoja, mimi namwamini Mungu sijui na siamini katika uchawi, mafanikio yangu ni Mungu tu na kujituma kwa bidii,” alisema Nisha.
Read more >>

NISHA AFUNGUKA MANENO MAZITO KWA WALE WOTE WANAOMWITA MCHAWI

MWANADADA kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amewabwatukia wasanii wenzake wanaomshutumu kwamba anatumia ndumba na kuwataka waache maneno hayo.
Mwanadada kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
Nisha aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kuzagaa kwa tetesi kuwa alizomewa na wasanii wenzake wakimwita mchawi kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa haraka kwenye sanaa, tofauti na wasanii wengine wanaosota kwa muda mrefu mpaka kupata mafanikio.
“Unajua siku zote mti wenye matunda ndiyo huwa unapigwa mawe, kipindi nikiwa bado sijaweza kucheza filamu zangu, yaani nikiwa chipukizi hakuna aliyekuwa ananizungumzia lakini sasa hivi wananiongelea kila kona, anayesema mimi ni mchawi basi huwa tunawanga pamoja, mimi namwamini Mungu sijui na siamini katika uchawi, mafanikio yangu ni Mungu tu na kujituma kwa bidii,” alisema Nisha.
Read more >>

MSANII NISHA WA BONGO MOVIE AMUANIKA WAZI BWANA’KE

 Supastaa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
MSANII wa filamu anayefanya poa na muvi yake ya Zena na Betina, Salma Jabu ‘Nisha’ amemnadi bwana’ake anayejulikana kwa jina la Fahad baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa amejichora ‘Mrs Fahad.’ 
Akizungumza na mwandishi wetu, Nisha alisema kuwa hawezi kuzungumza chochote kuhusiana na mchoro huo kwa sasa lakini siku si nyingi ukweli wote atauanika hadharani. 

“Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na hilo. Lakini hivi karibuni nitamtambulisha rasmi na itakuwa ‘ofisho’ watu wangu wa Global msiwe na wasi,” alisema Nisha.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger