MSANII WA BONGO ASUMBULIWA NA GONJWA BAYA

Oooh God! Mwigizaji wa kitambo kwenye tasnia ya maigizo Bongo, Augustino Mathias ‘Tino Madhahabu’ anasumbuliwa na gonjwa baya la moyo kwa zaidi ya miaka 7 akiwa hana msaada wowote kutoka kwa wasanii wenzake hivyo kulazimika kuomba msaada kwa Watanzania ambao anaamini wana moyo wa kusaidia.
Mwigizaji wa kitambo kwenye tasnia ya maigizo Bongo, Augustino Mathias ‘Tino Madhahabuna anayesumbuliwa na gonjwa baya la moyo kwa zaidi ya miaka 7.
Jamaa huyo alijipatia umaarufu mkubwa kupitia Kituo cha Televisioni cha TVT (wakati huo, kwa sasa TBC1) katika mchezo wa Bongo Dar es Salaam uliorushwa na kituo hicho miaka ya 2007, 2008 na kujinyakulia mashabiki wengi kutokana na aina ya kipekee ya uigizaji wake.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi, mwigizaji huyo alisema kuwa mwanzoni hakujua kama ana matatizo hayo ya moyo ingawa alikuwa na dalili za ugonjwa huo.
Augustino Mathias ‘Tino Madhahabuna' akiwa ametembelewa na mwandishi wa Global publishers, Deogratius Mongela.
“Nilikuwa nachoka mara kwa mara na muda mwingine kubanwa na pumzi na mapigo ya moyo kwenda mbio. Kuota nyama ndani ya pua na kuvimba miguu lakini nilijua ni hali ya kawaida kabisa nikawa naendelea na kazi za uigizaji bila kufahamu kuwa tatizo linakuwa kubwa.
“Ilifikia muda afya yangu ikazorota nikawa siwezi tena kufanya kazi ambazo zilikuwa zikiniingizia kipato cha kuendesha maisha kwa kuwa mimi ni baba wa watoto watano na familia yangu inanitegemea.
“Ndugu zangu kwa kweli ninateseka sana, imefikia hatua hata watu wangu wa karibu niliokuwa nikiwasaidia kwa mawazo, nao wamekuwa wananibeza kutokana na matatizo yangu ya kiafya,” alisimulia kwa majonzi makubwa na kuongeza:

Sehemu ya miguu ya msanii Augustino Mathias ‘Tino Madhahabuna' iliyovimba kutikana na ugonjwa wa moyo.
“Wasanii wana taarifa kuhusu matatizo yangu kiafya, lakini sijapata msaada wowote ule hata wa kimawazo au msanii kuja kunijulia hali.
“Kama wanashindwa kunisaidia kipindi hiki naumwa, wataweza kunisaidia nikifa?
“Daktari amenishauri nifanye mazoezi, amenielekeza vyakula kwa kipindi hiki, nazingatia hayo, nimekuwa naishi kwa kunyanyasika sana kama vile sina wenzangu (wasanii) hadi ndugu zangu wameamua kunisaidia kulea watoto wangu japokuwa wana maisha ya kawaida, hapa kodi na mahitaji mengine vinanisubiria.”

Kwa Mtanzania yeyote aliyeguswa na matatizo ya Tino Madhahabu anaweza kumsadia kupitia namba yake ya simu ambayo ni 0767 25 00 26 iliyosajiliwa kwa jina la Augustino Mathias. Kutoa ni moyo. 

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger