MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa
wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ
Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa
mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde
Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa
wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa
Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa
jina la Ally.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment