Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume,
amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama
hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.
Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda
hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua
waliyochukua.
Habari zinazohusiana
Habari zinazohusiana
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia
ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii
nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa
kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa
tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa
jinsia moja.
No comments:
Post a Comment