Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni
wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo
tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa
maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
1.Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi
hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika
kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.
Vigezo
hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale
ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu,
aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k.
Inaweza
kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna
wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo
mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.
2.Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo
tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata
ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado
huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi
ataishi maisha ya kifahari.
Hivyo
hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa
na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
3.Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili
ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na
haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini
anakupenda pia.
Wengi
katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni
kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
soma hii
Yeye
kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na
matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu
mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye
na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda
ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.
4.Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna
wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala
kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka.
Akija
wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo
atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta
maendeleo.
Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.
Hatimaye
inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji
lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena
katika soko.
5.Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani.
Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona
ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache
kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa
na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana.
Kitendo
hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi
kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama
maringo, dharau na kiburi.
6.Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana
mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa
hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa
zaidi.
Katika
kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri
wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na
miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
7.Maradhi hasa UKIMWI
Hili
kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu
wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na
mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana
wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa
ama kuwahi kuwa na mtoto.
Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.
8.Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo
linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali
mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi
hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa
maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya
kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
9.Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe
(pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile
kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso,
manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
-
Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya
lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama
mume kwake anaona kama ni utumwa.
10.Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale
wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya
kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa
ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi
hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na
uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
pitia na hii
No comments:
Post a Comment