STAA wa Bongo Fleva, Trey Revocatus ‘Baba Levo’
amedaiwa kumshushia kipigo shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Pili
Kimenya, mkazi wa Kisangani, Kigoma.
Kwa mujibu wa chanzo, Baba Levo alikwenda kwenye mazishi ya kaka yake
ambaye alikuwa mchumba wa Pili, Patrick Revocatus, baada ya kuzika
alimtuhumu shemeji yake huyo kuwa amemuibia marehemu cheni na aliposema
hajachukua, jamaa akampa kipigo.
Aliulizwa Baba Levo kuhusiana na tukio hilo alisema:“Hamna mimi
sikumpiga, wao na mama yake ndiyo walikuja kufanya fujo msibani
nikawafungulia mashtaka polisi. Mwanamke huyo alimharibia marehemu kwa
kumvutisha madawa ya kulevya.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment