BABY MADAHA AFULIA NA KUBAKI MWEUPE, HANA HATA SHILINGI MOJA

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umembana kiuchumi kwani kumbi nyingi za starehe zimefungwa kwa hiyo anashindwa kupata pesa.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
Akipiga stori mbili tatu baada ya kuvutiwa waya na mwandishi wa gazeti hili, Baby Madaha alisema kwa upande wake michongo yake mingi ya hela anaipata kupitia kumbi za starehe hivyo kwa sasa fedha haingii kabisa.
“Naomba Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uishe maana mtonyo umekata halafu sina namna ya kuingiza fedha zaidi ya muziki hivyo hali si hali kwa sasa jamani,” alisema Baby.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger