MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Abdulaziz
Chende ‘Dogo Janja’ (19) amewataka watu wanaomsema vibaya kuhusu kuwa na
uhusiano wa kimapenzi wamuache kwani anaonesha urijali wake.
Akistorisha na paparazi wetu, Dogo Janja alisema tangu aliponaswa
akiwa na demu wake amekuwa akisikia maneno ya kila aina ikiwa ni pamoja
na baadhi ya watu kusema kwamba ameanza mapenzi akiwa na umri mdogo kitu
ambacho hakubaliani nacho kwani wapo wasanii wenye umri kama wake
akiwemo Young D na Young Killer lakini watu hawawashangai.
“Mimi nawashangaa sana watu wanaonisema kwa sababu eti nina demu,
nimeamua kuonyesha urijali wangu au wanataka nigeuke shoga mbona wasanii
kibao ambao ninalingana nao wana wanawake?” alihoji Dogo Janja ambaye
sasa amerejea katika Kundi la Tip Top Connection alilokuwa amelikacha
kwa muda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment