BASI LA MORO BEST LAUA WATU ZAIDI YA 17 LEO HII


 Baadhi ya Miili ya Marehemu muda mchache baada ya kupata ajali kabla ya kupelekwa Hospitali.Basi hilo lilikuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es salaam



Watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la MORO BEST iliyotokea leo majira ya saa mbili asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio Basi hilo limegongana na lori katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma na kwamba miongoni mwa waliofariki ni pamoja na madereva na Makondakta wa magari yote mawili.

Hata hivyo chazo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa na wengine katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
 Baadhi ya wasamalia wema wakiwa wanaendelea kuokoa majeruhi na kuwaondoa waliofariki ,ambapo idaiwa watu zaidi ya watu 10 wamepoteza maisha
Hivi ndivyo basi lilivyo Haribika

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger