STAAwa sinema za
Kibongo, Lucy Komba, amedaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Klabu ya
Bongo Movie kwa kosa la kuwatolea lugha za kejeli.
Staa wa sinema za Kibongo, Lucy Komba,Alipotafutwa na paparazi wetu, Lucy ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha Septemba, mwaka huu, alisema hakumbuki kama aliwahi kuwakejeli wasanii hao isipokuwa wengi wamekuwa wakimjadili kwa suala hilo na sasa hawahudhurii kwenye vikao vya harusi yake.
“Mimi hata sikumbuki kama niliwahi kuongea hayo kwenye vyombo vya habari na kama niliongea labda walinielewa tofauti na kauli niliyoitoa, sioni sababu ya kuwekeana bifu ila kwa anayetaka acha aendelee,” alisema Lucy.

No comments:
Post a Comment