BIG boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu amemtolea uvivu
msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kwa kumwambia kuwa, alimkosea sana
marehemu Sheila Haule ‘Recho’ kwa kutomzika.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mtitu alisema marehemu Recho alikuwa
mtu wa kujitoa katika matatizo mbalimbali ukiwemo msiba wa mume wa
Wastara, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ lakini alishangaa kutomuona kwenye
msibani huo na alipomchana laivu akakasirika na kutangaza bifu.
“Nilimchana laivu kwani alimkosea marehemu, alipaswa kwenda kwani
hakuwa na sababu ya kueleweka zaidi ya kwenda bungeni kitu ambacho
angeweza kukiacha kikawakilishwa na mtu mwingine,” alisema Mtitu.Kwenye
utetezi wake juu ya kutoonekana msibani, Wastara alisema hakuwa na jinsi
kwani alikwenda bungeni mjini Dodoma kuwawakilisha wasanii wenzake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment