DIDA, KAMA VIPI AMUA KUWAPOTEZEA, KWANI HAWANA ISHU

KHADIJA Shaibu ni msichana anayefanya kazi kama yangu, yaani mwandishi, ingawa yeye yupo redioni. Kwa tulio katika fani kitambo kidogo, inakuwa rahisi zaidi kumfahamu kwa ile a.k.a yake, Dida wa Mchops. Hii ilitokana na ndoa yake ya kwanza.
Ni mdada anayeuacha usichana. Kikazi, Dida ni mzuri sana akiwa nyuma ya mic, hasa anapokuwa kwenye kile kipindi chake kilichompatia umaarufu mkubwa, cha Mitikisiko ya Pwani ndani ya Times FM, moja kati ya vituo vya redio vinavyofanya vizuri Tanzania.
Ingawa nina marafiki kadhaa watangazaji wa redio na televisheni, Dida si miongoni mwao. Hata hivyo, hii hainifanyi nishindwe kutambua na kuenzi uwezo wake, mashabiki wa muziki, hasa wa taarab, wanatambua ninamaanisha nini ninaposema kuhusu uwezo wake wa kuwalisha wasikilizaji wake kile wanachokitaka.
Nje ya kazi, Dida ni binadamu. Niwe mkweli, sijawahi kukutana na huyu dada, zaidi ninamuona kwenye tv, magazeti na mitandaoni tu. Lakini hata hivyo, ninajua kwa kiasi chake kuhusu sarakasi zake nje ya uwanja. Ni mtafutaji mzuri.
Ninahitaji sana kuzungumza na Dida kwenye eneo moja ambalo limempatia umaarufu mkubwa, la maisha yake ya kimapenzi. Sina uhakika hasa na umri wake kwa sasa, lakini kwa kumtazama, ni dada ambaye yupo njiani kuelekea miaka 40. Kwa maisha haya ya kila siku afadhali jana, si haba, yampasa kumshukuru Mungu kwani wengi waliishia njiani.
Kumbukumbu rasmi zinaonyesha Dida ameolewa na kuachika mara tatu. Baada ya ndoa yake ya kwanza  na Mohamed Mchopanga kuvunjika, alijaribu kwa Gervas Mbwiga na kushindwa kabla ya kuanguka tena katika ndoa yake ya tatu kwa Ezden Jumanne.
Nimewahi kusema mara nyingi kuwa ndoa ni fumbo kubwa, ambalo wenye uwezo wa kulifumbua ni wanandoa wenyewe. Wao ndiyo wanajua, kama hawaongei, kama wanalala mzungu wa nne, kama hawawapendi ndugu zao na kadhalika kwa sababu hayo yote yanapatikana katika ndoa.
Linapotokea tatizo katika ndoa ya mtu, usikimbilie kuhukumu, huwezi kujua, kaa kimya. Lakini inapokuja kuwa kama ilivyo kwa Dida, ni lazima uhisi uwepo wa tatizo upande wake. Haiwezekani, ndani ya miaka kumi ukawa na ndoa tatu zote zikikukataa.
Huenda kwa vile anaolewa na vijana wenzake? Hapana! Mumewe wa kwanza alikuwa mtu mzima na hata hawa wengine wawili, ujana una dhambi gani katika ndoa? Mbona kuna vijana wengi tu wamedumu katika ndoa zao?
Ninataka kumpa ushauri mdogo wa bure dada yangu Dida. Ninavyodhani, anachanganya maisha ya ndoa na ustaa. Yes, Dida ni staa, popote anapokwenda, ana-hang out na mastaa na pia anakaa nao jukwaa moja.
Wanawake wengi ni dhaifu wa ustaa, unawadanganya kwamba wanaweza kuwa juu ya wapenzi au waume zao, ndiyo maana unaona kuna ndoa chache sana za hawa mastaa zinazodumu. Kwa sababu ya ustaa wao, wanataka wajipangie ratiba zao, wafanye mambo yao kama wanavyotaka.
Ndiyo maana wanaume, hasa wa Kiafrika, wanaogopa kuwaoa mastaa, ni wasumbufu na wenye dharau, hasa kama watakuwa na vijisenti kidogo. Utamaduni wetu unakataa mambo haya, kwetu, mume ndiye kiongozi wa familia, hata kama utandawazi unajaribu kumpunguzia nguvu zake.
Ndoa yataka uvumilivu.

Lady Jaydee ni staa, mwenye jina na fedha pengine kuliko Dida, lakini hivi sasa anakimbiza mwaka wake wa kumi katika ndoa yake na staa mwenzake, Gardner G Habash.
Unadhani hawa hawana matatizo? Wanayo, lakini wanavumiliana, leo kikinuka, siku mbili tatu baadaye wanawekana sawa, wanasahau! Dida atafanya jambo la maana sana akiamua kuachana na ndoa kwa sababu nina uhakika hatampata mwanaume wa dizaini ya Bushoke, lakini anaweza kufurahia maisha ya kimapenzi bila kuolewa, kwani atakuwa huru kujiamulia anavyotaka!

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger