Mke wa ndoa wa marehemu Tyson, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ akiwa katika picha ya pamoja na mwanaye Sonia.
Kwa mujibu wa Monalisa, sherehe hiyo ni ya kimila kwa upande wa
kabila lao la Kizaramo ambapo wenyewe huita shughuli ya kuoshwa.Shughuli
hiyo iliyokusanya mastaa kibao ikiongozwa na Team Monalisa na Team
Natasha ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa, Yombo –
Buza jijini Dar es Salaam.Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na mwandishi wa habari hizi, wafiwa hao waliingizwa bafuni na kuogeshwa kisha kuvalishwa nguo mpya na kutolewa nje, zoezi ambalo lilifanyika chini ya usimamizi wa mkongwe wa maigizo nchini, Zawadi.
Muongozaji wa shughuli hiyo, Mama Abdul
alisema nia ya kuwaosha wafiwa hao ni mila na desturi ya Kabila la
Kizaramo na kwamba wao kama marafiki wa karibu waliamua kuwafanyia
wenzao kwa lengo la kuwapa moyo baada ya kuwa kwenye matatizo.
“Nguo na fedha tulizotoa hapa ni kuonyesha kuwa tunajua kuwa walikuwa
kwenye matatizo na sasa tunawapa nguvu ili waanze maisha yao mapya bila
ya mpendwa wao. Tunajua ni ngumu sana kibinadamu, ndiyo maana
tumesisitiza kuwa, dua ni muhimu kwa wenzetu,” alisema mama Abdul.VILIO UPYA
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
NATASHA ATOA NENO
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
“Pia tumefarijika sana na ujio wenu marafiki zetu. Tunajua mlikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini mmeona kuna umuhimu wa kuungana nasi na kutupa moyo. Mwenyezi Mungu awazidishie. Huu ndiyo urafiki wa kweli.”
No comments:
Post a Comment