Staa wa filamu za Kibongo, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ juzi kati
alimfanyia sapraizi ya kumpelekea keki baba yake wa kufikia Alex Humba
Lumila ambaye ni mume wa mama yake Suzan Lewis ‘Natasha’ katika siku
yake ya kuzaliwa.Staa huyo alifanya kisherehe hicho cha kushitukiza
kilichochukua nusu saa ikiwa ni katika kuonesha upendo wake kwake, hali
iliyomfanya mzee Humba abaki amepigwa na butwaa huku akionesha furaha
aliyokuwa nayo.
Mzee Alex Humba akimlisha keki mkewe Suzan Lewis ‘Natasha’.
Akizungumzia tukio hilo, mama wa Mona, Natasha alisema: “Nimefurahi
sana, namshukuru mtoto wangu Mona kwani sikutarajia kama atamfanyia baba
yake sherehe hii kwani hata mimi alinificha ila imeleta upendo mkubwa
ndani ya nyumba kama hivi unavyoona tunasherehekea.
Showing posts with label MONALISA. Show all posts
Showing posts with label MONALISA. Show all posts
MONALISA AMFANYIA SAPRAIZI BABA YAKE, FUATILIA ZAIDI HAPA
MONALISA AFANYIWA SHEREHE BAADA YA SIKU 40 ZA KIFO CHA MUMEWE
ZIKIWA zimekatika siku 40 tangu kifo cha muongozaji
maarufu Bongo, George Otieno ‘Tyson’, mke wa ndoa wa marehemu, Yvonne
Sheryl ‘Monalisa’, mama yake mzazi , Suzan Lewis ‘Natasha’ pamoja na
mwanaye Sonia wamefanyiwa sherehe.
Mke wa ndoa wa marehemu Tyson, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ akiwa katika picha ya pamoja na mwanaye Sonia.
Kwa mujibu wa Monalisa, sherehe hiyo ni ya kimila kwa upande wa
kabila lao la Kizaramo ambapo wenyewe huita shughuli ya kuoshwa.Shughuli
hiyo iliyokusanya mastaa kibao ikiongozwa na Team Monalisa na Team
Natasha ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa, Yombo –
Buza jijini Dar es Salaam.
Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na mwandishi wa habari hizi, wafiwa hao waliingizwa bafuni na kuogeshwa kisha kuvalishwa nguo mpya na kutolewa nje, zoezi ambalo lilifanyika chini ya usimamizi wa mkongwe wa maigizo nchini, Zawadi.
VILIO UPYA
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
NATASHA ATOA NENO
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
“Pia tumefarijika sana na ujio wenu marafiki zetu. Tunajua mlikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini mmeona kuna umuhimu wa kuungana nasi na kutupa moyo. Mwenyezi Mungu awazidishie. Huu ndiyo urafiki wa kweli.”
Read more >>

Muongozaji wa shughuli hiyo, Mama Abdul
alisema nia ya kuwaosha wafiwa hao ni mila na desturi ya Kabila la
Kizaramo na kwamba wao kama marafiki wa karibu waliamua kuwafanyia
wenzao kwa lengo la kuwapa moyo baada ya kuwa kwenye matatizo.
“Nguo na fedha tulizotoa hapa ni kuonyesha kuwa tunajua kuwa walikuwa
kwenye matatizo na sasa tunawapa nguvu ili waanze maisha yao mapya bila
ya mpendwa wao. Tunajua ni ngumu sana kibinadamu, ndiyo maana
tumesisitiza kuwa, dua ni muhimu kwa wenzetu,” alisema mama Abdul.VILIO UPYA
Katika shughuli hiyo, Monalisa alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio, hali iliyosababisha hata mwanaye Sonia aungane naye, lakini mashosti zake walimtuliza.
NATASHA ATOA NENO
Mama wa Monalisa, Natasha alisema: “Namshukuru sana Mungu kwa uwezo wake, kutujalia nguvu katika kipindi hiki kigumu kwa familia yetu, hasa mwanangu Monalisa na mwanaye Sonia.
“Pia tumefarijika sana na ujio wenu marafiki zetu. Tunajua mlikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini mmeona kuna umuhimu wa kuungana nasi na kutupa moyo. Mwenyezi Mungu awazidishie. Huu ndiyo urafiki wa kweli.”
Subscribe to:
Posts (Atom)