Imevuja! Mastaa wawili wa kike Bongo Muvi, Vivian
Minja na Najma wanadaiwa kutoleana maneno machafu kisha kuzichapa
kavukavu chanzo kikidaiwa eti walikuwa wakimgombea Mwenyekiti wa Klabu
ya Bongo Movies, Steven Mengere.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Vivian na Najma walifanya yao kwenye
hafla ya chakula cha usiku waliyokuwa wamealikwa na Steve iliyofanyika
kwenye Mgahawa wa Great Wall ulipo Masaki, Dar.
Ilidaiwa kuwa wawili
hao walianza kama utani lakini mambo yalipokolea, walijikuta wakipaza
sauti kabla ya kudundana huku wakimtaja Steve Nyerere kuwa wote ni watu
wake.
“Jamani Vivi na Najma wanagombea nini? Hapa kuna watu wanaojiheshimu,
wao hawaoni wanadhani wako kwenye Viwanja vya Leaders (Kinondoni)”
alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa eneo la tukio.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walimwendea hewani Vivian ambaye alikiri kutokea kwa ugomvi lakini hakupigana.
“Kweli ugomvi ulitokea, kwani maelewano yalivurugika kidogo na sababu
kubwa ilikuwa ni Najma kutajataja jina langu lakini mambo ya kumgombea
Steve si kweli watu wamezusha,” alisema Vivian.
Kwa upande wake
Najma alikuwa na haya ya kusema: “Vivi ndiye aliyeanza kunitukana na
mimi sijazoea kugombana na watu kwa sababu ninajiheshimu, nikawa
namfuata watu wakanishika, mimi sijawahi
kutembea na Steve na siwezi kutembea naye, ninajua vizuri tabia za
Bongo Movie za kuzungukana wao kwa wao, siwezi kuwa naye kwa sababu
wanaume matajiri wanaomtuma na kukaa nao mezani mmojawapo yupo mpenzi
wangu ambaye ananiweka mjini.
Baada ya Vivian kuzungumza, Steve Nyerere alimpigia mwandishi wetu na
kudai kuwa yeye alikwenda kuwapatanisha na kuzuia kugombana kwa sababu
yeye kama kiongozi ni kazi yake kufanya hivyo.
“Hivi nitakuwa na
akili gani kuwaita wanawake wawili ambao ninatoka nao sehemu moja? Huo
ni uzushi, hakuna kitu kama hicho kwani nina familia yangu,” alisema
Steve Nyerere.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment