Upinzani
wa jadi ni kitu cha kawaida sana kwenye mchezo wa soka duniani kote,
Tanzania kuna Simba vs Yanga, Uingereza kuna Manchester United vs
Liverpool, Misri kuna Al Ahly vs Zamalek, nchini Hispania kuna kubwa
kuliko ambayo inaingiza mpaka mambo ya kisiasa FC Barcelona vs watoto wa
mfalme Real Madrid.
Uhasama wa Real vs Barca ni mkubwa sana kiasi
cha hivi juzi nchini Marekani wakati wa mechi ya maandalizi ya msimu
mpya kati ya AS Roma dhidi ya Real Madrid, mizimu ya El Clasico
iliingilia mchezo huo wakati mchezaji wa zamani wa FC Barcelona Seydou
Keita alipokataa kushikana mikono na mchezaji wa Madrid – Pepe na kisha
akamrushia chupa ya maji kichwani kabla ya mechi.
Tukio
hili lilipelekea wachezaji wengine wa timu hizi mbili kuwatenganisha
wachezaji hao, Xabi Alonso akimtuliza mzuka Keita ambae alimtuhumu Pepe
kwa kumuita nyani kwenye mchezo wa kwanza wa Spanish Supercopa mwaka
2011.
Kwa mujibu wa Fox broadcast, kamisaa wa mchezo alikaririwa akisema kwamba Pepe alimpiga kibao Keita kwenye ugomvi huo.
Unaweza kuangalia video ya ugomvi wa Pepe vs Keita hapa chini…
No comments:
Post a Comment