NISHA: NIMECHEZEWA SANA NA WANAUME, KWA HIYO SITAWAAMINI TENA KATIKA MASUALA YA KIMAPENZI


Msanii wa Filamu za kibongo Salma Jabu 'Nisha' amedai kuwa hamjui mwanaume atakayeweza kuitwa baba wa watoto wake kwani kila mwanaume anayemtaka kimapenzi huwa haamini kama anaweza kutimiza hilo katika maisha yake ya mapenzi.....
Nisha alisema hivi sasa ni mapema sana kuwa na mawazo ya namna hiyo kwani bado anatafakari, na kudai hawezi kuweka asilimia nyingi wakati bado yeye ni kijana na anatafuta hela kwa sasa na si familia.....

"Nahitaji kuweka akili chini kwa sababu ishu ya kuzaa au kuwa na mwanaume ambaye anaweza kulea watoto si kitu kidogo, ni lazima akili yangu itulie na ifanye maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu vinginevyo naweza kulia kwa sababu sitakuwa na maamuzi sahihi ambayo yatanifanya niishi kwa raha," alisema Nisha.

Muigizaji huyo tangu aanze kupata jina amevurugwa na wanaume kadhaa kimapenzi akiwemo staa wa bongo fleva Ney wa Mitego, ambaye uhusiano wao ulionekana kama wa kutaka kiki kabla ya kutemana ghafla

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger