Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa
Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya
Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho
baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha
mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala la Wema kukashifiwa
liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Wema
wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa Instagram kwamba ni kwa
nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno jukwaani (hivi karibuni
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya kumfungulia biashara ya
maana?
“Tujaribuni kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu
Diamond. Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno
namna ile kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye
ni mfuasi wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa
kumshauri ‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha
zinazomuonesha Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata
mauno jukwaani kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.
WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau hao walimtaka Wema
kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy Sumari (2005),
Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi kwa jinsi
wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza kuendesha maisha
yao bila kudhalilishwa majukwaani.
WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team
Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema
kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na
uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata
mauno.
DIAMOND AWAJIBU
Baada ya wadau hao kumshauri
Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo walidai yanamdhalilisha,
kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond alishindwa kuvumilia
ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka wake unaodaiwa
kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond alieleza kwamba yeye
kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu kama mpenzi wake na
suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.
WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri ningewaona kweli mna
akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu (Wema) kama mngemshauri
apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida,
huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta
maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe, mimi kama bwana, wajibu
wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala
vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. “Waswahili wanasema
mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji
safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo anatakiwa aamue kunywa maji!
“Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza
nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi
zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama
nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu,
nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”
WAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya waraka huo, mashabiki
na wadau waliopo kwenye mtandao huo walimgeukia Diamond kwa kumlaumu
kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona amemfungulia dada yake Esma
Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa akimtumia tu bila faida
yoyote?
MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana na waraka huo,
aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika wa kwake na
kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.
MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada ya meneja huyo kubwanga
manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu
na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na penzi hilo la mwanaye
ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha hivyo anaacha
‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.
“Jamani sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao
wazungushane wee mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa
WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo
imemchanganya.
TUJIKUMBUSHE
Penzi la Wema na Diamond limekuwa
likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi
cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana,
kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel
Mungilwa ‘Penny’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment