Lile ndinga aina ya Toyota Vitz la mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’
ambalo lilidaiwa kutumika kwa ujambazi juzikati, bado lina ugumu wa
kuachiwa kutokana na watuhumiwa walioka matwa nalo kuhusishwa na makosa
ya mauaji.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka jeshi la polisi ambacho kiliomba
hifadhi ya jina, Dude amekuwa akifuatilia mara kadhaa Kituo cha Polisi
cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar, lakini imeshi ndikana kutokana na kosa
hilo.
“Hili suala limeshakuwa gumu, si jepesi kama anavyofikiria, hili gari
halipati leo wala kesho atasubiri sana maana wale watuhumiwa
waliohusika na lile tukio la kutaka kuiba Bajaj ni majambazi sugu,
walikuwa wakisakwa kwa kesi ya mauaji,” kilisema chanzo hicho.
Ndinga hilo lilikamatwa Julai 21, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama
likiwa na watuhumiwa waliohusika na tukio la wizi wa Bajaj
waliojitambulisha kwa majina ya Seif na Longina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment