
A.Y tayari ameshafika Marekani na wameanza kwa kukutana na Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval.
Huu msafara wa wasanii kutoka Africa unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y ambapo kesho wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama.

Hata kina Ay wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend.




No comments:
Post a Comment