Kikongwe huyo alikutwa na gazeti hili hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.
Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo.
Uwazi lilishuhudia sehemu kubwa ya ukuta wa nyumba anayoishi kikongwe huyo ikiwa imemeguka kwa ajili ya kuchimbuliwa na kuliwa.
Majirani walilieleza gazeti hili kwamba, nyumba anayoishi kikongwe huyo aliachiwa kuilinda na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Musada karibu miaka 20 iliyopita bila kupewa huduma nyingine zikiwemo fedha.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed Katungi akikabidhi msaada wa chakula kwa Bw. Athuman Kulaba.
Akizungumza na Uwazi kwa lugha ya Kisukuma, kikongwe huyo alikiri
kuwepo kwenye nyumba hiyo kwa miaka 20. Alisema awali alikuwa akipewa
pesa na tajiri yake lakini baadaye utaratibu huo ukafa hivyo kwa sababu
ya kukosa pesa ya kujikumu ndiyo akaamua kula vyakula vya ajabu, ukiwemo
udongo wa ukuta wa nyumba hiyo.
Bw.
Athuman Kulaba amkishukuru mwandishi kutoka Global, Bw Denis Mtima
(kulia) pamoja na Menyekiti (Mohamed Katungi) kwa msaada alioupata.
Alisema anawashukuru majirani wa eneo hilo ambao wameweza kutambua
maisha magumu anayoishi na kuamua kumpeleka hospitali na kumsaidia
chakula.“Kwa sasa naomba Watanzania wenzangu wanisaidie nauli ili niweze
kurudi kwetu Bukene, Tabora, maisha hapa ni magumu sana,” alisema
kikongwe huyo.Kwa Watanzania watakaoguswa na maisha magumu ya mzee huyo wanaweza kumsaidia nauli kwa kutumia namba ya simu ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed Katungi 0784 295833 au 0715 295833.
No comments:
Post a Comment