NEY WA MITEGO: NILISHUHUDIA KWA MACHO YANGU MSANII WA BONGO MOVIE AKIJIUZA

MKALI wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, amesema kuwa aliwahi kushuhudia staa mmoja wa filamu Bongo (jina tunalo) akijiuza kwa mgeni mmoja kutoka nje ya nchi na kwamba tukio kama hilo aliliona zaidi ya mara moja.
Msanii wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego akipozi.
Akizungumza na gazeti hili mapema juzi, Nay mkali wa nyimbo za Nakula ujana na Muziki Gani, alisema mabinti wengi wanacheza filamu siyo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha, bali wanafanya hivyo ili kuuza sura ambayo baadaye huitumia kwa ajili ya kujiuza ili kujiingizia kipato.
“Mimi kila kitu ambacho huwa ninakiimba huwa kina ukweli ndani yake na niko tayari kwa mtu ambaye atahisi nimemuonea tutafikishana popote pale, nilishawahi kushuhudia mabinti wa bongo movie wakinunuliwa na wageni wanaokuja kutoka nje ya nchi,” alisema Nay.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger