Showing posts with label NEY WA MITEGO. Show all posts
Showing posts with label NEY WA MITEGO. Show all posts

NAY WA MITEGO AKIRI KUJIHUSISHA NA UFREEMASON, ALIYOYASEMA YOTE YASOME HAPA

Rapper Nay wa Mitego ambaye hivi karibuni alizusha maneno mengi kutokana na video ya wimbo wake  yenye mambo ya kutisha, amewajibu mashabiki wake kwamba hajali kuhusishwa na ufreemason ilimradi anaingiza pesa anayoitaka.Akizungumza na kituo cha redio cha Victoria FM kilichopo mjini Musoma, Nay amesema amekuwa akipokea maswali mengi yakitaka kujua kama anajihusisha na jamii ya siri ya freemason kutokana na matendo yake.


Mimi sijali kama najihusisha na freemason, naangalia jinsi gani naingiza pesa  na huu ndio aina ya muziki wangu na kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. Muziki wangu na maisha yangu kama yanahusishwa na freemason lakini ninachojali ni pesa tu, alisema
Read more >>

NAY WA MITEGO AKIRI KUZAA NA MSANII WA BONGO MUVI, PA AMWANIKA MTOTO WALIOZAA

Mambo hadharani! Baada ya kimya kirefu, staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mara ya kwanza amemwanika mtoto aliyezaa na msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na kukiri kwamba ni wa kwake.
Mtoto wa staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nay alisema kuwa anampenda mwanaye huyo na kwa sasa anaishi naye nyumbani kwake. Kimara-Baruti, Dar na ana umri wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Mama mzazi wa Munie ambaye ni msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ akipozi.
“Nampenda sana mwanangu ndiyo maana nimeamua kumchukua kwa mama yake Skaina na kuja kumlea kwangu, analelewa vizuri sana na mama yake ambaye ni Siwema namshukuru Mungu mwanangu anaendelea kukua, nafurahia sana kukaa na mwanangu karibu tofauti na alivyokuwa kwa mama yake,” alisema Nay wa Mitego.
‘Nay wa Mitego’ akiwa na mwanaye.
Skaina aliwahi kukiri kuwa mwananye huyo baba yake ni Nay lakini baada ya Nay kuulizwa alichengachenga hivyo sasa ameamua kumuweka wazi.
Read more >>

WAJUA KUA NEY NDO CHANZO CHA DIAMOND KUHAIRISHA KUMUOA WEMA??? SOMA CHANZO HAPA


IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki.


Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’Ushauri huo umekuwa mwiba kwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu ambaye amekuwa na ndoto yakuolewa na staa huyo anayekimbiza kitaani na wimbo wake wa Mdogomdogo.Wema Sepetu akiwa na mpenzi wake 'Diamond Platinum'.Akifafanua zaidi kuhusiana na ushauri huo, Nay alisema: “Kuna mifano mingi sana nimeiona kutoka kwa wasanii ambao wameoa, wengi wao wameshasanda sasa mdogo wangu (Diamond) na yeye alipoleta hoja ya kutaka kuoa nikaona sasa anatafuta shimo la kwenda kujifukia, nikamshauri aache.”
Read more >>

SKENDO: JACK WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA NAY


Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia madai ya kutoka na msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na kudai kuwa wao ni washikaji tu ila ukaribu wao umesababisha mtifuano kati yake na mchumba wake, Siwema.

Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum Nay alisema, watu wamekuwa wakieneza kuwa yeye na Wolper wanatoka kiasi cha kumkosesha amani Siwema na kufikia wakati f’lani wakatibuana.
Mahojiano kati ya mwandishi wetu na Nay yalikuwa hivi:
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.

Ijumaa: Kuna madai kuwa wewe unatoka na Wolper, hii ikoje? Nay: Wolper ni mshikaji wangu, kama watu wanavyojua kwamba yule ana mambo ya kisela f’lani na hicho ndicho kinanifanya nimpende. Ila najua kitu kilichowafanya watu wahisi kuna kitu kati yangu na yeye ni baada ya kuposti picha yangu kwenye ukurasa wake wa Insta na hapo ndipo likaibuka tatizo. Na hilo lilileta ugomvi kwenye uhusiano wangu lakini ukweli ni kwamba kama mahusiano yapo ni ya kawaida tu.

Nay wa Mitego akiwa na mchumba wake, Siwema. Ijumaa: Sasa wewe na Wolper mkikutana huwa mnazungumzia nini?

Nay: Mambo ya kazi tu, si unajua nina mpango wa kucheza muvi baadaye.

Ijumaa: Mbona sasa inadaiwa mnatoka kwa siri?

Nay: Hayo maneno ya watu tu japokuwa ni mwanamke mzuri, anamvutia mwanaume yoyote rijali
Ijumaa: Ikitokea ameingia mzimamzima kwako itakuwaje?

Nay: Ikitokea ameamua kuingia mzimamzima, nitaangalia mapokeo yake (Kicheko sanaaa)
Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana. Tukimpata naye tutampa nafasi ya kufunguka.
Read more >>

NAY WA MITEGO: NILIKUWA MWIZI BALAA, SOMA HISTORIA YAKE HAPA

CONFESSION! Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili wa maisha yake kuwa kabla hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!
Akizungumza na paparazi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la kulala katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia kufanya matukio ya uhalifu.

Staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
“Kwanza kabisa nilikuwa nalala Feri na watoto machokoraa. Nilikuwa naona ndiyo maisha japokuwa nilijua kuna maisha mengine mazuri zaidi lakini ningeyapate?
“Dah! Yaani kusema kweli nilipita kwenye majanga makubwa sana jamani! Anyway, kimsingi ukweli wa maisha yangu siwezi kuuficha maana nitakuwa najiongopea bure kwani ni kweli niliishi katika maisha ya matukio sana,” alisema Nay.
Akizidi kutiririka mbele ya kinasa sauti cha Amani, Nay ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mr Nay aliweka bayana kwamba kwa nyakati tofauti aliwahi kuiba  vitu mbalimbali (hakupenda kuvitaja) kwa watu wa karibu yake akiwemo Prodyuza Paul Mathysse ‘P Funk’ na kwenye studio moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.
“Enzi zangu nilikuwa balaa, Majani mwenyewe (P. Funk) nilishawahi kumliza, nakumbuka pia kuna jamaa zangu walikuwa na studio ya muziki pale Mwenge nao niliwapiga.
“Tena hawa jamaa wa studio nakumbuka walikuja kinitaiti nikiwa kwenye msiba, wakanitia pingu na kunipeleka kituo cha polisi lakini bahati nzuri marehemu John Mjema, alikuwa mshikaji wangu sana, akaja kunitoa,” alisema Nay.

'Nay wa Mitego’ akifanya shoo.
John Mjema ‘Bomba la Mvua’ alikuwa mwanamuziki wa Kizazi Kipya, alifariki dunia Februari 10, 2008 kwa kujichoma kisu cha shingo nyumbani kwake Mtoni Kijichi jijini Dar.
Nay akaongeza: “Kulala polisi nadhani ni kama mara saba hivi na mara zote aliyekuwa akinitoa ni John Mjema. Yeye wakati ule alikuwa akifanya kazi kule maeneo ya Feri.
Pamoja na matukio hayo ambayo Nay ameyafanya, alisema alishatubu na kumwomba Mungu amsamehe kwani anaamini ujana ndiyo ulikuwa ukimsumbua.
“Yaliyopita si ndwele, kwa sasa naganga yajayo maana muziki unanilipa na naendelea na harakati zangu kama kawaida, nilishasahau hayo matukio ya ajabuajabu,” alimaliza Nay.
Miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata msanii huyo kupitia muziki wa Bongo Fleva ni kujenga nyumba Kimara-Rombo jijini Dar na gari la kutembelea aina ya Nissan Murano.
Read more >>

NEY WA MITEGO: NILISHUHUDIA KWA MACHO YANGU MSANII WA BONGO MOVIE AKIJIUZA

MKALI wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, amesema kuwa aliwahi kushuhudia staa mmoja wa filamu Bongo (jina tunalo) akijiuza kwa mgeni mmoja kutoka nje ya nchi na kwamba tukio kama hilo aliliona zaidi ya mara moja.
Msanii wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego akipozi.
Akizungumza na gazeti hili mapema juzi, Nay mkali wa nyimbo za Nakula ujana na Muziki Gani, alisema mabinti wengi wanacheza filamu siyo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha, bali wanafanya hivyo ili kuuza sura ambayo baadaye huitumia kwa ajili ya kujiuza ili kujiingizia kipato.
“Mimi kila kitu ambacho huwa ninakiimba huwa kina ukweli ndani yake na niko tayari kwa mtu ambaye atahisi nimemuonea tutafikishana popote pale, nilishawahi kushuhudia mabinti wa bongo movie wakinunuliwa na wageni wanaokuja kutoka nje ya nchi,” alisema Nay.
Read more >>

PICHA ZA NEY WA MITEGO AKIWA NA DEMU WAKE CHUMBANI

Read more >>

NEY WA MITEGO NI MUONGO MKUBWA, KUMBE HANA NYUMBA 3 KAMA ALIVYOTAMBA. SOMA UKWELI HAPA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_gGTVHjnCQ3ylO775iI4feK8gIONdTgHsgAx4qlK7yMxRMK1PRTptHF9vUpw3xAk2XsygmpPffh0tsbz5083CS0x2yaLDIq6EuXPqj3HCdaqB7SplkG94my8eK6wSYUD9Un7A0nOj_Us/s1600/10456457_939160349431717_5429598818210293882_n.jpg
Miezi miwili iliyopita msanii Ney wa mitego alianika utajiri wa ajabu zikiwemo nyumba nne na gari moja ya kisasa nissan murano!! Akichezesha taya na mwandishi wetu aliyekuwa manager wa ney amesema tangu aachane na ney miezi 7 iliyopita alikuwa hana hata nyumba moja ameshangaa kumuona ana nyumba nne ghafla lakini manager amesema inawezekana jamaa anatafuta kiki ili watu wanaomuita kwenye show wafikirie kumpa mpunga mrefu na si laki laki wanazolipwa kwenye fiesta! Amefunguka kwamba Ney kuwa na hizo nyumba basi itakuwa ni miujiza.
Read more >>

HII NDIO NYUMBA ALIYOJENGA NEY WA MITEGO, TENA ANAHAMIA LEO RASMI, IONE HAPA

Msanii Ney wa Mitego ameingia katika Headlines chache za Wasaniii waliojenga nyumba na kuhamia mwaka 2014.
image-13-06-14-08-07
image-13-06-14-08-07-1
image-13-06-14-08-07-2
image-13-06-14-08-07-3
image-13-06-14-08-07-5
image-13-06-14-08-07-4
image-13-06-14-08-07-6
image-13-06-14-08-07-7
image-13-06-14-08-07-8
image-13-06-14-08-07-9
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia, BOFYA HAPA
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger