ALIYEKUWA mchumba wa
marehemu Rachel Haule ‘Recho’, George Saguda amesema ameamua kupeleka
mali zote za marehemu kwa ndugu zake ili wao wajue utaratibu wa
kuzitumia.
Akizungumza na paparazi wetu, Saguda alisema kwa sasa hahusiki na
suala la mirathi ya Recho japo alikuwa akiishi na marehemu kama mke wake
na kudai kuwa mali zote zilizokuwa zinamhusu Recho, tayari amezikabidhi
kwa ndugu zake.
“Marehemu Recho nilikuwa nikiishi naye kama mke wangu lakini mali
zake zote nimeshazikabidhi kwa ndugu zake kwa sababu wao ndiyo
wanaohusika na suala zima la mirathi endapo kutakuwa na ulazima wa
kunishirikisha basi wataniambia,” alisema Saguda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment