Showing posts with label mastaa. Show all posts
Showing posts with label mastaa. Show all posts

BIA MOJA YASABABISHA MTANGAZAJI HANIFA HAMIDU KUTIWA MBARONI KWA KUTAKA KUUA.


RB namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILIkwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar, imemtia mbaroni mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu wa baa aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu anayetuhumiwa kumshambuli mhudumu wa baa.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita kwenye baa maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta, Dar.
Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Mhudumu wa baa anayetambulika kwa jina la Aika Andrew (32) aliyenusurika kuuawa na mtangazaji maarufu Bongo, 'Lady Hanifa' .

Kwa mujibu wa mashuhuda, katika tukio hilo lililojiri mishale ya saa 11:00 jioni, Hanifa alipofika aliingia moja kwa moja jikoni kuangalia biashara yake kisha akarudi kukaa sehemu ya baa.

Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu.

Majeraha ya moto shingoni mwa Aika Andrew.

Ilidaiwa kwamba alimwita mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha aliyokuwa akidai Aika lakini muda huohuo Lady Hanifa  akaanza kudai chenji yake kwa mabavu.

Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.

Wasamaria wema wakimpeleka Hospitali ya Mwananyamala, Aika Andrew.

Iliendelea kudaiwa kwamba katika purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu alimchoma nacho Aika tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa akimuunguza shingoni kwa kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya moto kisha wakakimbia.

Habari zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia Kituo cha Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema walifika katika kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu mwili mzima.

Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.

CREDITS:GPL
Read more >>

SAGUDA AKABIDHI MALI ZOTE ZA RECHO UKWENI

ALIYEKUWA mchumba wa marehemu Rachel Haule ‘Recho’, George Saguda amesema ameamua kupeleka mali zote za marehemu kwa ndugu zake ili wao wajue utaratibu wa kuzitumia.
George Saguda akiwa na aliekuwa mchumba wake marehemu Rachel Haule ‘Recho’
Akizungumza na paparazi wetu, Saguda alisema kwa sasa hahusiki na suala la mirathi ya Recho japo alikuwa akiishi na marehemu kama mke wake na kudai kuwa mali zote zilizokuwa zinamhusu Recho, tayari amezikabidhi kwa ndugu zake.
“Marehemu Recho nilikuwa nikiishi naye kama mke wangu lakini mali zake zote nimeshazikabidhi kwa ndugu zake kwa sababu wao ndiyo wanaohusika na suala zima la mirathi endapo kutakuwa na ulazima wa kunishirikisha basi wataniambia,” alisema Saguda.
Read more >>

MARTIN KADINDA ANUNUA SAA YENYE THAMANI YA TSH. MILION 15, IONE HAPA HIYO SAA

Hii ndio habari ya mujini, haya kama ulikuwa hujui basi chukua hii, designer mkubwa wa nguo Tanzania ameamua kufunguka kupitia mtandao wako wa jamii wa makubwa haya blog yakuwa yeye gari kwake sio ki2, kwa kudhihirisha hilo ameamua kununua saa inayoitwa TAGHEURE yenye thamani ya $9800 ambayo ni sawa sawa na milion 14 za kitanzania na hii ndio kauli aliyoitoa designer martin kadinda kutokana na saa hiyo....Yeeeeeeeeees I finaly own one…. #TAGHeuer #GrandCarrera watch….. U own fancy car I own this Watch……. Google it if u dont mind.. Its all about uamuzi,design n fashion..big up kwa martin kadinda coz u have done something different in the industry of Tanzania keep it up jamany u really desearve to be congratulated
Read more >>

PICHA HAPA JINSI NDOA YA MWISHO MWAMPAMBA ILIVYOFUNGWA



Read more >>

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA MWANADADA MREMBO AGNESS MASOGANGE.


Jokate atupia picha mitandao ya kijamii akiwa anataka kuliwa uroda, angalia mwenyewe alichofanyiwa hapa===>>http://mdadisitz.blogspot.com/2014/09/laana-jokate-atupia-picha-mitandaoni.html
Read more >>

NYUMBA YA SPIKA WA BUNGE ILIYOGHARIMU TAKLIBANI BILION 1.5


Uzunguni nje kidogo ya Dodoma mjini imegharimu takribani Tshs 1.5 Billion na imejengwa na kampuni ya Pacha Building Construction Company. Hii inakuwa nyumba ya kwanza rasmi ya Spika kwani hapo awali hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika.
Read more >>

MZUNGU KICHAA AFUNGUKA TETESI YEYE KUTOKA KIMAPENZI NA SALAMA, SOMA ZAIDI HAPA

 
Mzungu Kichaa amekanusha uvumi huo na
kusema hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na Salama.
“Sio kweli mimi si-date na Salama Jabir” Alisema
alipohojiwa na katika kipindi cha TV cha Sporah,
“tulifanya kazi pamoja kama majaji katika kipindi
cha TV (BSS), so kuna vitu vingi ambavyo
tunafanana pia alisoma UK na ni mtu mzuri, so ni
marafiki tu kulikuwa na uvumi ulisambaa kwenye
media”.
Salama Jabir
Pamoja na kuwa hakuna ukweli wowote juu ya
swala hilo lakini Mzungu Kichaa amedai kuwa kuna
mtu aliwahi kumuuliza kama ana uhusiano na
Salama na alimjibu ndio lakini hakumaanisha.
Mzungu Kichaa katika Sporah show
“kuna mtu aliniuliza nikiwa uwanja wa ndege,
Mzungu Kichaa ni kweli una uhusiano nae, ilinibidi
niseme ndio kwasababu nilikuwa nacheka sababu
ilikuwa ni idea ya kuchekesha kwamba Mzungu
Kichaa ana uhusiano na Salama.” Alisema Mzungu
Kichaa.
Akiuzungumzia uhusiano wake na Salama
amesema,
“Sisi sio best friends so sio kwamba tunatoka sana
pamoja, ninayo namba yake, na yeye lazima
atakuwa nayo ya kwangu lakini hatutumiani
ujumbe kila wakati.”
Katika hali ya utani mzungu Kichaa alisema:
“People thought it was really funny and they got
excited about it because imagine if these two, the
crazy white man and the crazy Salama, coz Salama
is crazy imagine if those two have children how
crazy they will be.”
Aliongeza kuwa baada ya kusikia
kinachozungumzwa mitaani aliwasiliana na Salama
kumjulisha,
“Nilimtumia barua pepe kumwambia kile
kinachosemwa na watu ili asije kushtuka akija
kusikia”.
Read more >>

MSHINDI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO AWA KIVUTIO MITAA YA KARIAKOO‏

Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.
Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.
Read more >>

MAKALIO YA KICHINA YAMUUMBUA SUPER STAA HUYU WA MJINI, SOMA KIOJA HIKI CHA MWAKA

 
Oops! wahenga walisema ajali haina kinga........ 

Blac Chyna ni afiki yake kipenzi na TV star kim kardashian  na pia ni mama mtoto wa rapperTyga. Mdada huyo ambaye zamani alikuwa ni stripper, amekuwa ni gumzo kwa muda mrefu kutokana na makalio yake ambayo watu wengi wanasema ni ya bandia yaani fake.

Lakini mrembo humbo ambaye kwa sasa ni model, alikanusha uvumi huo na kusema makalio yake ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Yaliyojiri hivi karibuni, ni kwamba makalio hayo yalianza kuporomoka taratibu wakati anatembea na alipigwa picha akijaribu kuyafunika na sweta.

Inasemekana dada huyo alioneka akikimbilia kwa dotka kwa ajili ya marekebisho ya fasta.....majanga!!

Watu wanasema makalio ya Kim yanaweza kuwa bandia pia―Samaki mmoja akioza, wote wameoza heheh
Read more >>

WAFAHAMU WANAWAKE WAREMBO SANA NCHINI KENYA.

Kutokana na Uchunguzi uliofanywana mtandao mmoja huko Kenya, umeeleza kuwa Kenya ni moja ya nchi yenye wanawake wazuri sana waliojaliwa, tena baadhi yao ni wafanyakazi katika Vyombo vya habari.



Sasa hapa tunapozungumzia madem ambao wameumbika katika hidara zote ndani na nje huko kenya ni lazima uwataje Madem hawa ambao kila kukicha wamekuwa wakizungumziwa katika vyombo mbalimbali vya habari na kufuatiliwa kwa karibu sana. kutokana tu na Uzuri walionao.

Kwa mujibu wa misemo mingi ya watu wengi kwamba Mwanamke akishazaa ama kupata mtoto, kitu ambacho kinatokea ni kwamba mwanamke hupoteza uzuri na uhalisia wa umbo lake la kawaida. sasa hawa nitakaowataja hapa  ni tayari wameshazaa lakini cha kushangaza ni kuwa Bado maumbo yao yanaongezeka mvuto kila siku!! Kati ya wasichana hao ni pamoja na.

1. Sheila Mwanyigah
\
This lady has been holding it down since the days Before Ghafla and she's still got it like an 8 month pregnant lass!

2. Corazon




3. Avril
Pity she has a taste for South African cooking! That figure? Heh! It makes sense. No questions asked! And if there are any, the answer is Avril's figure! Who is the hottest singer? Avril's figure! Who did God's Chosen Blogger turn to for inspiration? Avril's figure.


5. Grace Msalame


6. Vera Sidika
Read more >>

WOLPER NI FULL USAFI, SHUHUDIA HAPA BRD ANALOLALA WOLPER DAH NI UTAMU

Katika kile kinachoonyesha kwamba msanii wa bongo movie jack wolper sio msafi tu wa mwili na kutupia pamba kali, hii nyingine imeonyesha wazi jinsi gani mwanadada huyu ni mtanashati, hii ni baada ya kufanikiwa kupata mandhari ya chumba chake na kitanda jinsi vinavuvyoshawishi kulala kabisa, tazama hapa picha
Read more >>

MWAULID KITENGE AONDOKA RASMI REDIO ONE, SOMA ALICHOKIANDIKA HAPA


Maulid Kitenge.
MTANGAZAJI wa michezo wa Radio One Stereo, Maulid Kitenge kupitia akaunti yake ya Twitter hivi punde ametangaza kuondoka rasmi katika radio hiyo baada 
ya kuitumikia kwa miaka 14. Kupitia Twitter, Kitenge ameandika hivi:

Read more >>

MUONE DEMU WA MILARD AYO

Read more >>

MUONE SALAMA JABIR AKIWA KATUPIA NGUO ZA KIKE; CHEKI PICHA HAPA

wengi tumezoea kumuona salama katika mavazi ya kiume . je umewahi kumuona salama akiwa katupia kike zaidi, kumbe anapendeza zaidi kuliko akivaa kiume, tazama picha hizi utakubari


Read more >>

Watangazaji Kibonde na Gadner Habash Wapandishwa Kizimbani

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.

Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.

Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena.
Read more >>

BBA THE CHASE: ONEAL WA BOTSWANA AOMBA KUMCHUMBIA FEZA WA TANZANIA

Huenda siku si nyingi tunaweza kuanza kuimba ‘mlisema haolewi mbona kaolewa’ baada ya Oneal kumtaka uchumba wa kweli kweli Feza Kessy.
LgScreen-ShotOnealFeza2_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_001302150017487
Katika kazi waliyokuwa wamepewa kufanya mjengoni humo, Oneal aliamua kupiga magoti wakati akimwaga sera za nguvu kwa Feza na kumwambia kuwa maisha yake yalikuwa shagala bagala kabla hajakutana na mwakilishi huyo wa Tanzania.
Maneno hayo matamu yalimwingia vyema Feza ambaye alikuwa akitabasamu muda wote kuashiria upendo mzito kwa jamaa huyo wa Botswana ambaye anataka wawe na maisha pamoja siku za usoni.
Wasiriki wengine waliamka na kuwashangalia wapenzi hao kama yalivyo maisha ya kawaida. Kazi hiyo ilionekana kuchukua picha ya ukweli hasa kwa wale ambao wameyaweka wazi mahusiano yao.
Kumbuka Nando ni miongoni mwa washiriki waliotajwa kutoka wiki hii, mpigie kura kumuokoa.
Read more >>

LAANA: MTOTO WA MIEZI MIWILI ANAJISIWA...!!

Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kutokea nchini licha ya kupigwa vita kwa kampeni mbalimbali

Baadhi ya ukatili huo ni pamoja na kubakwa na ule wa kukatwa viungo vya mwili kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino).


Licha ya kupigiwa kelele, hata kampeni mbalimbali za kupinga kufanyika, unyama huo umeendelea kufanyika na tukio la hivi karibuni limemhusisha mtoto Erisia Tito mwenye miezi miwili anayedaiwa kunajisiwa wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.


Tukio hilo limekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali wilayani humo, huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa linahusiana na imani za kishirikina.


Unaweza kujiuliza maswali mengi, hata inakuwaje mtoto wa miezi miwili kunajisiwa?

 


Katika vijiwe vya kahawa wilayani Mpwapwa, hii ni habari kubwa zilizokuwa zikizungumzwa kuhusu kunajisiwa kwa mtoto huyo swali likibaki; Je, yule mtu alimnajisi mtoto ameishia wapi?

Naingia chumba cha Mganga Mkuu Wilaya ya Mpwapwa kupata maelezo ya mtoto huyo tangu alipofikishwa katika hospitali ya wilaya hiyo, maendeleo yaliyofikiwa na utaratibu wa kiuchunguzi unavyoendelea.


Kauli ya Mganga Mkuu

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Lunemo Sakafu anasema kuwa tangu alipolazwa, mtoto huyo alikuwa akipelekwa kliniki kwa ajili ya kupatiwa chanzo mbalimbali na kupima afya yake, kwamba alikuwa na afya nzuri.

“Hakuzaliwa katika hospitali hii ila alikuwa akihudhuria kliniki, alizaliwa kwa wakunga wa jadi na mara ya mwisho kuja hapa hospitali ilikuwa Aprili 15, mwaka huu na alikuwa na afya nzuri,” alisema


Ashangazwa

Alisema kuwa alishangazwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo alipofikishwa kwa mara nyingine katika hospitali hiyo kwani alikuwa akitokwa haja zote bila kikomo.

“Tunampatia matibabu ya kina ili kujua tatizo ni nini. Kwa sasa tuna utaratibu wa kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ili akafanyiwe vipimo vya kina kwa kuwa mtoto huyu anatoa haja zote bila kikomo,” anasema Sakafu.


Sakafu anasema hata wazazi wa mtoto huyo walipoulizwa juu ya hali aliyonayo mtoto wao, walipishana kauli katika maelezo yao na kwamba jambo hilo liliwatia shaka.


Kauli za wazazi

Baba wa mtoto huyo, Silvani Msemakweli anasema kuwa tangu mtoto wake alipozaliwa alikuwa na maumivu wakati wa kupata haja kubwa.

“Tangu alipozaliwa hali hii ilikuwapo hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa mtoto analia, kwani husikia maumivu makali. Katika ukoo wetu yupo mmoja wa ndugu zetu aliyewahi kuwa na mtoto aliyekumbwa na hali kama hii ya mtoto wangu,” anasema na kuongeza:


“Yeye alipona baada ya kutumia dawa za kienyeji na alipona kabisa, siyo kweli kuwa mtoto alinajisiwa.”


Msemakweli anaongeza kuwa ni vigumu kuamini kama mtoto huyo amenajisiwa kutokana na mazingira ya familia hizo mbili, yaani familia yake na ya mke wake.


“Japo sikuwapo siku hiyo, lakini bado siamini kama mtoto wangu atakuwa amenajisiwa. Kwa sasa mama yangu ndiyo anayeshikiliwa na polisi na kufunguliwa kesi,” anasema Msemakweli.


Mama wa mtoto huyo, Rejina Msemakweli anasema kuwa yeye alijifungua kwa mkunga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Hilda Maderemo na kwamba mtoto alikuwa mzima na hakuwa na tatizo lolote.


Anasema kuwa baada ya kujifungua alianza kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya kupata chanjo mbalimbali.


“Mwanangu nilimzaa akiwa mzima nilishangaa siku moja analia sana wakati huo alikuwa amepakatwa na bibi yake,” anasema na anaongeza:


“Nilimwacha na bibi yake kwa kuwa nilikwenda shambani ila niliporudi nilimkuta akiwa analia kupita kiasi. Nilimchukua na kumwogesha, lakini kabla sijamaliza niligundua kuwa ameumia sehemu zake za siri na alikuwa akitoka kinyesi mfululizo, yaani mbele na nyuma.”


Regina anaeleza kuwa familia yake ina watoto wawili ambao wote ni wasichana, mume wake pamoja na mdogo wake wa kike, kwamba pia wanaishi kwa ukaribu mkubwa na familia ya mume wake.


“Katika maisha yetu nimekuwa nikiishi na wakwe zangu bila maelewano mazuri, familia imekuwa ni yenye kugombana kila wakati, hata kama kitu ni kidogo. Lakini yataibuka mambo makubwa kiasi kwamba utadhani ni watu wasio familia moja inaniuma sana,” alisikitisha.


“Naongea kwa kuvumilia tu, lakini moyoni ninaumia kwa kiasi kikubwa kuona mwanangu amekuwa katika hali kama hii sielewi. Tukijaribu kumwuliza mama mkwe wangu hasemi ukweli kuwa mtoto amekuwaje,” anasimulia Regina huku akilia machozi.


Anasema kuwa aligundua kwamba sehemu za siri za mtoto wake zimevimba na kuonyesha kukwaruzika huku akitokwa na kinyesi bila kikomo.


Kauli ya mkunga

Mkunga Hilda Mademo anakiri kuwa alimzalisha Regina na kwamba mtoto huyo alikuwa mzima bila kuwa na kasoro yoyote.

“Mimi ndiye niliyemzalisha mama huyo na mtoto alizaliwa akiwa mzima kabisa. Suala la kupatikana kwa tatizo hilo, ukweli wanao wazazi wenyewe. Huduma zangu nilizitoa hata hospitali ya wilaya inalifahamu, walinitembelea hadi hapa kuona mazingira ninayofanyia kazi na kunisaidia baadhi ya vifaa kwa mfano haya mabakuli,” anasema Hilda.


Polisi yatoa tamko

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi David Misime anakiri kupokea taarifa za kunajisiwa kwa mtoto wa miezi miwili katika Kijiji cha Ising’u wilayani Mpwapwa.

“Sisi tulipokea taarifa hiyo na kuanza kuifanyia kazi za awali, hadi sasa bibi wa mtoto huyo yuko mikononi mwa polisi. Tunasubiri jibu la kitaalamu kutoka kwa daktari kwa kuwa wakati mtoto amepelekwa katika hospitali,”alisema Misime na kuongeza:



“Katika Kituo cha Polisi hapakuwa na ushahidi wa kujitosheleza kwa kuwa mtoto huyo tayari alikwishasafishwa siku tatu zilizopita.”

Viongozi wa Serikali wakemea

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, Ryoba Kangoye amekemea vikali tukio hilo na kuliita ni la ugaidi kwa kuwa mtu huyo hakuwa na nia ya kubaka bali ni kuua.

“Hii hali siyo ya kawaida ni mstuko mkubwa kusikia hili kama hiyo kujitokeza katika mazingira hayo. Hivi, Mtanzania wa leo kufikia kufanya jambo kama hilo ni ajabu kubwa, hata hiyo familia kukaa kimya ni kunyima haki vyombo vya sheria kufanya kazi zake na kupoteza ushahidi uliokamika,“ anasema Kangoye.


Mtendaji wa kijiji hicho, Emmanuel Mamba anasema kuwa waliposikia tukio hilo walijikuta ni kama wamemwagiwa maji au tindikali wakilifananisha na mauaji.


“Tulioposikia tuliishiwa na nguvu kwa kuwa hata kama matendo kama hayo hufanyika, basi isingekuwa kwa mtoto mdogo kama huyo, asiye na uwezo wowote ule. Tulijiuliza maswali mengi hata kuhisi huenda walitaka kumfanyia ukeketaji,” anasema Mamba


Viongozi wa dini

Kwa niaba ya madhebu ya dini, Padiri Masasi Deo kutoka Kanisa la Katoliki Mpwapwa, amekemea vikali tabia hiyo akisema:

“Nionavyo sasa umefika wakati wa watu wenye dhamana na jamii kukaa pamoja na kufanya ibada na kujua mbinu mpya ya kufundisha maadili kutokana na hali ya maadili ilivyobadilika nchini.”


Haki za binadamu

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu (AFNET)Mkoa wa Dodoma, Sara Mwanga amesema kuwa kitendo hiko ni unyama na kwamba jamii bado haina elimu ya kujitambua kuhusu ukatili unaofanywa hasa katika kushughulikia kesi za aina hiyo.

“Watoto wengi wamekuwa wakiumizwa, lakini mwishowe hakuna linalofanyika katika kumtetea mtoto huyo kutokana na wahalifu huachiwa huru kwa kile kinachodaiwa ushahidi haujakamilika. Kwa kweli kuna utata mkubwa katika suala hilo,” alisisitiza.


Aliitaka Serikali kupitia vyombo vya dola kuwa makini katika kuangalia namna ya kupatikana kwa ushahidi ili kutenda haki kwa watoto wanapoumizwa, badala ya watuhumiwa kuachiwa huru kwa madai kuwa ushahidi haujakamilika.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger