Showing posts with label CHID BENZ. Show all posts
Showing posts with label CHID BENZ. Show all posts

RAY C: NAHAKIKISHA CHID BENZ ANAKWENDA JELA

NYOTA wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa kupokea kipigo cha maana kutoka kwa msanii mwenzake, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz, ameibuka na kudai kuwa atahakikisha rapa huyo anaozea jela kwa kitendo hicho alichomfanyia.
Nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizungumza na gazeti hili, Ray C alisema amejikuta akipatwa na dhamira hiyo kutokana na msanii huyo, licha ya yeye mwenyewe na mama yake kumpigia simu za kutaka amsamehe, lakini anakana mbele za watu anapoulizwa, tena hadi redioni.
“Chid na mama yake wamenipigia simu kutaka nimsamehe lakini ninashindwa kwa sababu akiulizwa na watu anakataa hajanipiga, sasa kama hajanipiga anaomba msamaha wa nini, nimekwenda kwao na polisi kama mara tano lakini haonekani, inaonekana amejificha sehemu, mimi nasema awaonee haohao wasiojua sheria,” alisema msanii huyo ambaye hivi sasa anaendesha vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz.
Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Chid Benz mwenye tuzo tano za Kili, licha ya kukiri kumpigia Ray C simu pamoja na mama yake, alikataa kupiga kwa ajili ya kuomba msamaha kwa sababu hakumpiga msichana huyo mkongwe katika Bongo Fleva.
“Mimi nimpige Ray C? Halafu achubuke mguuni? Chid Benz angempiga angepasuka sura na angevimba kila sehemu. Yeye anajua nini kilitokea lakini anasema maneno yasiyokuwepo ilimradi apate huruma ya watu. Nilishamkataza kuwa karibu na mzazi mwenzangu kwa kuwa najua kampuni yake haina future.
“Mbona hasemi kama nilishawahi kwenda pale na kumweleza sitaki na akaniomba msamaha?
“Mimi sikumpiga, mchubuko alioupata ni mchecheto wake tu baada ya kujikwaa na kuanguka wakati akinikimbia, mimi nichukue cheni? Hayo ni mambo ya kizamani kwamba mtu ukimpatia sababu unasema amechukua pesa sijui na nini, siwezi kuchukua cheni ya Ray C, kwa maisha gani aliyonayo?

“Anasema nilimpigia simu kumuomba radhi, ni kweli lakini siyo kumwomba radhi, nilimpigia na kumwambia tuachane na haya mambo, sisi wote tunaonekana mateja tu mbele za watu ambao tumeshindwana huko sasa tunataka publicity.
“Wanaosema mimi ni mkorofi hawanijui, kama ni hivyo mbona ile kesi ya kumpiga msichana kule Ilala nimeshinda?” alihoji Chid Benz.
Read more >>

CHID BENZ AMBUTUA MANGUMI RAY C, HABARI KAMILI IPO HAPA

evu! Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.
Mwanaisha aliyepigwa na Chidi Benz hapo awali.
CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C  Changanyikeni.
UNGA WATAJWA
Sosi wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C, wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.
KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
Sehemu ya damu chumbani kwa Ray C kutokana na kipigo cha Chidi Benz..
“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.
RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio kwa kipigo kikali walichopokea.
RAY C AVUJA DAMU
“Ray C aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.
RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.
“Alinipiga vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo ambalo lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu hadi kuja kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye nilitoka naye ofisini kwangu.
“Ujue jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na Mariam, sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.
“Huko nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada ya kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za kuondoa sumu.
“Tumeendelea kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna baadhi ya kazi nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu. Pia alishawahi kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa alikataa na kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai mimi ndiyo namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.
“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”
SOO LIPO POLISI
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.
Juhudi za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi anaweza kutupigia.
CHID BENZ NI TATIZO?
Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.
Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger