Showing posts with label JINI KABULA. Show all posts
Showing posts with label JINI KABULA. Show all posts

JINI KABULA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU PENZI LAKE NA BUSHOKE

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya penzi lake na msanii Maximilian Bushoke kuwa na sarakasi nyingi lakini anaamini atamuoa.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Akizungumza na paparazi wetu, Jini alisema watu wengi wamekuwa wakiuponda uhusiano wake kwa kuwa Bushoke anaishi Afrika Kusini na kuona hakuna mapenzi ya kweli lakini ukweli anaoujua yeye ndoa ipo.
Msanii wa Bongo Fleva Maximilian Bushoke.
“Piga ua garagaza, Bushoke ndiye mwanaume ambaye anajua kunipa tiba nzuri ya mapenzi, hakuna mwingine, atanioa tu kwa sababu sioni kipingamizi,” alisema Jini Kabula.
Read more >>

AMA KWELI JINI KABULA NI CHANGUDOA WAKUTUPWA, ANGALIA USHENZI ALIOSEMA KUHUSU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA VIMINI VYAKE

STAA wa sinema za Kibongo, Miriam Mjolwa ‘Jini Kabula’ amecharuka baada ya kukosolewa juu ya mavazi ya mitego, vimini, anayovaa ndani ya mwezi wa Ramadhani.
Staa wa sinema za Kibongo, Miriam Mjolwa ‘Jini Kabula’
Baada ya majirani wanaofunga kufikisha malalamiko, paparazi wetu alimvutia waya Jini Kabula na kumsomea mashtaka hayo ambapo alisema kuwa alikuwa lokesheni siku waliyomuona lakini pia hahofii sana kwani mwezi huo haumuhusu.
“Hao wanaweka chumvi tu mimi sikuwepo huko mtaani nilikuwa lokesheni tangu mwezi uanze, na hata kama nitavaa nguo za ajabu, mwezi huu haunihusu nitavaa vyovyote nipendavyo,” alisema Jini Kabula.
Read more >>

JINI KABULA: HAKUNA STAA AMBAE HAJAWAHI KUKANYAGA KWA DOKTA KAMDEGE

staa wa filamu za kibongo nchini Miliamu Jorwa Jini Kabula amesema ameibuka na kusema haamini kama kuna staa yeyote nchini ambae amefanikiwa kimaisha bila kupitia kwa Dokta Kamdege kupta baraka zake.

Akiongea na gazeti hili Miliamu Jorwa alisema kuwa" Mganga wa mstaa nchini amewasaidia nikiwemo mimi mwenyewe na kama kuna mtu akisema hajawahi kukanyaga kwake huyo muongo na mnafiki kabisa" Aliasema Jini Kabura

Aidha msanii huyo anasema mganga huyo anaetibu kupitia miti shamba alimsaidia sana wakati anaanza kupata jina kwani kulikuwa na ushindani mkubwa sana wa kupata majina na mafanikio bila nguvu zake za ziada basi hali ingekuwa mbaya hadi leo.

Mganga huyo ambae anatibu maelfu ya watu kutumia miti shamba huku akiwawezesha wengi kuwa na mafanikio kupitia sanaa, kazi, biashara nk na tayari hata raia toka nchi za nje wamekuwa wakitua nchini na kumfuata huko aliko.

Hata hivyo kwa sasa mganga huyo yupo Jijini Dar na watu wafanyabishara wengi wamekuwa wakimiminika Kiwalani alikofikia kwa ajili kuwasawazishiwa mambo yao na ameendelea kutoa uwito kwa wakazi wa Jiji la Dar kuendelea kufika kwake kwani hana siku nyingi ataondoka kuelekea Uturuki alikoitwa na Serikali ya huko.

Mganga huyo anatibu magonjwa mengi tu pamoja kumsafisha mtu kupanda cheo, kuolewa, kufanikiwa kibiashara na mambo mengine na anatibu kutumia miti shamba na hata kama uko nje ya nchi atakusaidia ukiwa huko huko na ametaja namba yake ya simu kwa watakaopenda kumtafuta 0788-844490 na moja kwa moja ataongea nae.

Read more >>

JINI KABULA: ANAYENITAKA KIMAHABA BASI ANIFUATE NYUMBANI NA SIO KUKUTANA BAR


Sitaki  tena....Ndivyo  unavyoweza  kusema  kutokana  na kauli  ya  nyota  wa filamu  za  kibongo  Mirium Jolwa  "Jini Kabula"  ambaye  amedai  kuwa  kwa  sasa  hataki  kusikia  mapenzi  ya  pesa  na  kama  kuna  mwanaume  anayemtaka  basi  amfuate  nyumbani  na  si  kuitana  baa.....

Kabula  alisema  kuwa  wanaume  wengi  wamekuwa  na  tabia  ya  kuitana  baa  huku  wakihisi  kuwa  kila  mwanamke  ni  mlevi  kutokana  na  tabia  ya  baadhi  ya  wasanii  ambao  wamekuwa  wakijirahisisha  kwa  kupewa  pombe...
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger