Showing posts with label PENNY. Show all posts
Showing posts with label PENNY. Show all posts

PENNY AMWEKA HADHARANI MCHUMBA WAKE, TAZAMA PICHA HAPA

Picha nyingine Penny akionyesha pete yake laivu pasipo na kupepesa
Mtangazaji wa 93.7 EFM Radio, Penny Mungilwa , ameposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na  pete inayosemekana amevishwa na mchumba wake mpya siku za hivi karibuni, ingawa bado yeye mwenyewe hajaweka wazi kuhusiana na jambo hilo.
Picha nyingine Penny akionyesha pete yake laivu pasipo na kupepesa
Read more >>

PENNY: MSINISHANGAE KUFUNGA RAMADHANI, KWANI FAMILIA YANGUA HUAMINI MUNGU NI MMOJA

MTANGAZAJI wa Redio  EFM aliyewahi kuanguka kimahaba na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amewafungukia wanaomshangaa kuhusu kufunga mwezi wa Ramadhani na kuwataka watu hao wasimshangae kuhusiana na jambo hilo.
Mtangazaji wa Redio  EFM,Penniel Mungilwa ‘Penny’a
Akifafanua ishu hiyo mbele ya mwandishi wetu, staa huyo alisema kuwa amezaliwa katika familia yenye dini mbili japokuwa yeye ni Mkristo, lakini hufunga Ramadhani na Kwaresma sambamba na kusheherekea sikukuu zote kwa kuwa familia yao huamini Mungu ni mmoja.
Read more >>

RAMADHANI IMESAIDIA KUMALIZA BIFU LA WEMA, PENNY!

STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”
Mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Read more >>

PENNY ACHUMBIWA, AONESHA PETE YA UCHUMBA INSTAGRAM, SOMA ZAIDI HAPA


Mtangazaji wa kipindi cha Genge cha EFM Radio, Penniel Mwingilwa 'VJ Penny'.
Penniel Mwingilwa amepost kwenye Instagram picha inayoonesha mkono wake wa kushoto ukiwa juu ya usukani wa gari ambao una pete katika kidole cha chanda.
“Mdogo hicho nini kwenye kidolee?? Kabla sijaanza kurukaruka kwa furaha,”amehoji mmoja wa followers wake.
“Hv kumbe ni kweli @vjpenny04 ume engage? Kuna sehemu nilickia, basi sawa hongera zako mpe hi @halimakimwana1,” ameandika mwingine.
“Mungu awaondoshee hasad za waja wenye chuki za roho,ameenRabilaallamin @vjpenny94@halimakimwana1, na Kama ukweli uko engaged mwanangu mie furaha tele hapa nasubiri invitation card yangu ya mr&mrs na tutakuja all the way from Uk kwa jinsi nilivyo na hamu nayolove u all wanawake wenye msimamo, “amechangia mwingine.
Katika maelezo ya picha hiyo, Penny amesema; “Road trip…site here we come… Cc @halimakimwana1.”

Read more >>

ANGALIA PENNY ALIVYOKUWA ANAMPA DIAMOND MAMBO MATAMU, YAANI NI SHIDAA

 Kila mtu anaithamini na kuipenda tarehe ya siku 
yake ya kuzaliwa,ni siku ambayo baadhi yetu huifurahia kwa
 mitindo tofauti tofauti kulingamna 

na nafasi aliyonayo mtu husika,lakini hebu
 jiulize how it feels ndani ya hiyo siku mhimu kabisa 
unapofanyiwa kitu kizuri na cha pekee na mtu
 mhimu maishani mwako,inapendeza siyo?hivyo ndivyo
 nilivyojiskia siku ya jana baada ya 
kufanyiwa suprise ya  birthday party
 na kipenzi changu,Penniel pamoja
 na Mama yangu mpenzi,dada yangu Esma,Halima kimwana 
na familia yangu kwa ujumla.
checkout picha zikijieleze zenyewe........
Ilikuwa ni baada ya kutoka kwenye 
uzinduzi wa Coke studio,kufika nyumbani 
Nikapokelewa kwa bashasha na Dada angu Queen Darlin(aliyeshikilia cake)
Dada angu Esma na mmoja wa rafiki wa familia yangu pamoja na Shilole nae alikuwep kusapoti
Baby akanisuprise kwa Kiss mwanana kabisa , like duuuh!!!
Nyakati kaama hizi mamabo ya maakuri kama hivi huwa hayakosekani
My dada,Queen Darlin
Na tuwaache washangae!!!!
Mambo yakahamia chumbani sasa . wooow!!
Kupendwa ndio huku..Mtoto wa bi Sandra mie

Read more >>

WEMA, PENNY NI BALAA, SOMA MWENYEWE HAPA

Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake. 

 Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV. 

Kwa mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake. 

Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua kama Wema alikuwepo. “Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea, 

Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza: 
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.” Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. 

Alipopatikana, alijibu hivi: “Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.” 

Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka: “Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.” 
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake
Read more >>

MSHIKEMSHIKE: PENNY, WEMA WAKUMBANA STUDIO


Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.

Mtangazaji wa Dtv Penniel Mungilwa ‘Penny’
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua kama Wema alikuwepo.
“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea, Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo Wema Sepetu.
Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.”

Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake.
Read more >>

ANGALIA UREMBO ALONAO PENNY HAPA


Read more >>

PENNY AKANA UVUMI KUHUSU MAHUSIANO MAPYA YA KIMAPENZI BAADA YA DIAMOND

Baada ya kuachana na Diamond Platnumz, Peniel  Mwingila aka Vj Penny ameendelea mbele na  maisha yake, lakini amekanusha kuwa na mpenzi mpya kama ambavyo wengi wamekuwa wakidhani hasa wanapomuona yuko karibu na mwanaume mwingine.
Leo Penny ameamua kuvunja ukimya wake na kukanusha habari zilizoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ana mpenzi mpya aitwaye Rummy, hiki ndicho alichokiandika: “Ah come on people!!?? Kweli mi ni mkimya ila  sasa mnavuka mipaka, seriously?? Am so disappointed to see posts that Rummy is my new  boyfriend..mnatoa wapi hizi rumours? Just  because sijibu shutuma natupiwaga haimanishi mimi sio binadamu kila siku mnanizushia mapya  its not funny maisha yangu kutwa mnayafanya uwanja wa kutunga kitu, yes mnatukana na hakuna tusi jipya nawaacha ili mjifurahishe but  now u r crossing the line, I have alot of respect  for Rummy he is my homeboy na marafiki pia wa kiume nisiwe nao? Wengi wanajua rummy ni nani  yangu ila making these stories aint cool at all.
Enough has a limit! Nitukaneni all u want ila msinisingizie vitu sijafanya its just not fair at all.  Kama new boyfriend ntaweka mwenyewe mapenzi  hayajifichi ila tusizushiane uongo, nayavumilia  mengi ila hili too much.”
Read more >>

HIVI NDIVYO JINSI WEMA NA PENNY WALIVYOIHARIBU FAMILIA YA DIAMOND

Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili Bongo, mwigizaji Wema Isaac Sepetu na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wanadaiwa kuipasua familia ya kinara wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
 
Wema akiwa na Diamond Platinum.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu na familia hiyo kuna mgawanyiko ambao umesababisha mpasuko unaofanya familia hiyo kuwa na makundi mawili yasiyoelewana juu ya uhusiano wa Diamond na warembo hao.
 
Penny kushoto katika Pozi tofauti tofauti na mashosti zake.
Kwa sasa Diamond anatoka kimapenzi na Wema baada ya kumwagana na Penny lakini mtangazaji huyo anadaiwa kuendelea kwenda katika familia hiyo kwani asilimia kubwa inaonesha anakubalika zaidi ya wengine wote.
 
Mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akipozi.
TEAM PENNY VS TEAM WEMA
Habari zilidai kuwa mpasuko huo ni mkubwa kwani kundi moja linalojiita Team Penny linamkubali zaidi Penny na lingine ambalo lina watu wachache Team Wema linamkubali Wema. Imefahamika kwamba kundi linalomkubali Penny na kumuona ndiye mwanamke sahihi kuwa na Diamond japokuwa wameshaachana ni Mama Diamond mwenyewe, Sanura Kassim ‘Sandra’, dada zake Esma Platnumz, Queen Darleen, Anko na dada wa hiyari wa Diamond, Halima Haroun ‘Kimwana’.

 
Wema akiwa na Rommy Jones.
Ilidaiwa kwamba kundi hilo limekuwa likitoa ushirikiano wa karibu mno kwa Penny na sehemu nyingi wanakuwa wote ikiwemo kwenye sherehe na viwanja vya starehe, yaani ni fulu kujiachia.
Habari hizo zilidadavua kuwa hata dada wa Diamond, Esma anaishi nyumba moja na wifi yake huyo wa zamani.

 
Mama Diamond Sanura Kassim ‘Sandra’ akiwa na Penny.
“Familia ya Diamond imegawanyika katika makundi mawili, kundi kubwa linamkubali sana Penny japokuwa alishaachana na Diamond. Ilisemekana kuwa si familia tu kwani hata madansa wa Diamond wanampenda sana Penny kuliko Wema,” kilisema chanzo.
 
Baba Diamond, Abdul Jumaa.
TEAM WEMA HII HAPA
Uchunguzi wa wanahabari wetu ulibaini kuwa ndani ya kundi linalomtaka Wema kuna watu wachache akiwemo Diamond mwenyewe, baba yake, Abdul Jumaa ambaye kwa upande wake alitamka wazi: “Wema ndiye mkwe wa ukweli kabisa.”

Baba huyo alikwenda mbali na kusema anamkubali Wema kwa sababu ana nyota kali na ana roho nzuri hivyo akiendelea kuwa na mwanaye atakuwa na mafanikio tofauti na alivyokuwa na Penny.
Pia ilijulikana kuwa kundi hilo lina mtu mwingine, ndugu wa Diamond aitwaye Rommy Jones ambaye amekuwa akionekana na Wema mara kwa mara hasa wakati msanii huyo akiwa amesafiri.

HALIMA KIMWANA AITWA KIGEUGEU
Taarifa nyingine zilidai kwamba katika sakata hilo, Halima kimwana amekuwa akiitwa kigeugeu kutokana na kutokuwa na upande anaosimamia. “Mara utamuona na Wema ghafla unamuona tena na Penny, yule hata haeleweki. Anajichetua sana,” kilisema chanzo chetu.

MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
 “Mimi siwezi kumchagulia Diamond mwanamke wa kuwa naye, yeye mwenyewe ataamua kwa sababu ni mtu mzima kwa hiyo siwezi kumpangia au kumchagulia mwanamke wa kuwa naye,” alisema mama Diamond bila kukanusha kuwa na ukaribu zaidi na Penny.

MSIKIE HALIMA KIMWANA
Baada ya kuwatafuta Diamond, Wema na Penny bila mafanikio, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Halima Kimwana ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Sisi tuko karibu na Penny kwa sababu anapenda kujichanganya na sisi hivyo hata Wema akija kutuchukua na kutaka twende naye klabu hatukatai kwa sababu wote ni mawifi zetu.
“Hatubagui kwani hakuna siku ambayo Wema alishataka kuwa na sisi tukamkatalia.”

MASWALI
Hivi karibuni picha za Penny akiwa na mawifi zake kwenye shughuli ya kumtoa mtoto wa ndugu yao zilivuja ambapo ndani ya sherehe hiyo pia Diamond alikuwepo akiwa anacheza dufu lakini Wema hakuonekana, jambo lililozua maswali.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger