FLORA ASEMA KAMA ANGEMKOSA H. BABA, BASI ANGEPATA SHIDA KIMAISHA

UA la Bongo Movies, Flora Mvungi amefunguka kuwa anashukuru Mungu kumpata mume mwema, Hamisi Baba ‘H.Baba’ kwani vinginevyo angeyumba kimaisha.
Flora Mvungi na mumewe H. Baba.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Flora alisema H. Baba ni mwanaume anayestahili sifa zote hivyo endapo angekutana na mwanaume mwingine basi angeyaona mapenzi machungu.“Mungu hakukosea kuniletea H. Baba, nampenda sana kwani ni mtu anayenijali mimi na mtoto wetu Tanzanite yaani sijui kitu gani ambacho nakikosa kwake, bila huyu maisha yangeyumba,” alisema Flora.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger