MAN CITY YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA CHELSE,

BAO: Ivanovic akipiga shuti lililoipatia Chelsea bao pekee la ushindi dhidi ya Manchester City.
FURAHA: Ivanovic (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Chelsea.
THE SPECIAL ONE: Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akifurahia ushindi wa timu yake.
HAPITI MTU: Kipa wa Chelsea, Petr Cech na Gary Cahill wakimdhibiti Alvaro Negredo wa Man City.
TIMU ya Chelsea imeibuka na pointi tatu muhimu katika Uwanja wa Etihad baada ya kuilaza Manchester City bao 1-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England usiku huu.
Bao pekee la Chelsea limewekwa kimiani na Ivanovic dakika ya 32 ya mchezo. Kwa matokeo hayo, Chelsea sasa wana pointi 53 wakiwa nafasi ya tatu huku Manchester City wakiwa nafasi ya pili na pointi 53 wakitofautiana na Chelsea kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Arsenal wanaendelea kubaki kileleni wakiwa na pointi 55 kibindoni baada ya kucheza michezo 24.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger