BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo,
marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama
Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.
Akipiga stori na paparazi wetu, Baba Kanumba alisema anashangazwa na
tabia ya mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini
Shinyanga ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.
“Namshangaa mama Kanumba ni njaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha
ukoo wa Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila
sababu za msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.
Akijibu tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote
aende mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani
mimi si mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba
nilijiendea tu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment