Fumanizi hilo liliripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari, ‘VUNJA JUNGU GESTI’ ambapo Huruma alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni, Dar.
Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.
Katika tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa
na chanzo chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa
anaishi maeneo ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye
nyumba huyo ili kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.Wanahabari wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe wakibeba vitu ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.
“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma.
Alisema kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa umalizike Machi Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na bifu kubwa kiasi cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.
Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi jamaa huyo alidai alitekwa.
No comments:
Post a Comment