MOYO unauma! Staa wa R&B Bongo, Juma Khalid ‘Jux
Vuitton’ amekiri kuteswa na ishu ya mwanamitindo Jacqueline Fitzpatric
Cliff ‘Jack Patrick’ akiomba asiulizwe habari za modo huyo aliyekuwa
mpenzi wake ambaye kwa sasa yupo nyuma ya nondo kwa madai ya kukamatwa
na madawa ya kulevya ‘unga’ huko Macau, Hong Kong nchini China.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, jamaa huyo alisema kuwa kwa sasa
hapendi kabisa kusikia mtu akimuuliza habari zinazohusiana na mpenzi
wake huyo, kwani zinamtoa kwenye ‘mudi’ na badala yake ana mambo mengi
ya kuzungumza.
“Naomba mtu asiniulize ishu za Jack, zinanitibua na zimeshazungumzwa
sana hivyo sioni kipya cha kuzungumzia zaidi ya muziki wangu, kwa sasa
nina projekti mpya kibao zinakuja,” alisema Jux anayetamba na ngoma ya
Nitasubiri aliyomuimbia Jack.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment