Mafanikio! Taarifa ikufikie kuwa staa wa Bongo
Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ amekanusha stori za madai ya kuhongwa gari
jipya analosukuma mjini kwa sasa aina ya Toyota Mark X.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Linah ambaye hivi karibuni alitokea
nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo wake mpya alisema mkoko huo
amepewa na kampuni anayofanya nayo kazi ya NFZ.
“Nani kasema nimehongwa gari? Siwezi kuhongwa gari kwani najituma
sana kwemye kazi yangu,” alisema Linah.Mbali na kumiliki ndinga hilo,
miezi kadhaa iliyopita aliwajengea nyumba wazazi wake na sasa anajenga
ya kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment