RAFIKI zangu, karibuni tena uwanjani kwa ajili ya kuongeza ujuzi katika
maisha yetu ya uhusiano. Ndugu zangu, maua usipoyamwagilia maji na
kuyatia mbolea yatakauka na kudumaa.
Hata mapenzi nayo ni hivyo hivyo, lazima kila siku upate wasaa wa kujifunza kuwa bora zaidi kwa mpenzi wako.
Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba, maisha yetu yametawaliwa
zaidi na mapenzi. Utaishi na mpenzi wako katika ndoa, kuzaa naye watoto
na mambo mengine mengi.
Ikiwa utashindwa kuishi na mwenzi wako ni wazi kwamba kila kitu katika
maisha yako hakitaenda vyema. Hivyo basi, ni wajibu wetu kujifunza kila
kukicha juu ya mapenzi.
Wiki mbili zilizopita, nilianza sehemu ya kwanza ya mada hii kama
inavyoonekana hapo juu, lakini wiki jana niliiacha kiporo kupisha mada
iliyohusu Sikukuu ya Valentine, ilikuwa mada nzito, iliyosindikizwa na
Love Messages kali zilizoongeza nakshi katika sikukuu hiyo. Pia nilitoa
somo (kwa njia ya simu) la namna ya kufanya bonge la massage ya
kimahaba kwa mwandani wako..
Tutaendelea.
No comments:
Post a Comment