HAPPY! Staa aliyeibuliwa na Shindalo la Vaa, Imba na
Cheza Kama Rihanna lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers,
Wellu Sengo amefunguka kuwa anainjoi kuwa mama kwani ameanza
kuheshimika.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Wellu alisema amejifungua mwanaye
aliyempa jina la Valempia hivi karibuni japo bado hajafunga ndoa lakini
anaamini heshima ya kuwa mama kwake ni kitu cha kujivunia.
“Sijutii
kuwa mama, hayo mambo ya ndoa ni mipango ya Mungu. Najivunia kuwa mama
na ni heshima kubwa ambayo pia naiona kama nisingekuwa naye,
nisingeipata,” alisema Wellu.
Wellu, baada ya kuibuliwa na Global Publishers, alijitosa kwenye Bongo Movies na kufanya vizuri hadi sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment