Kumbe! Sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amefunguka kwamba amewajua wabaya wake wanaomfuatilia na
kumsakama kwa ubaya katika maisha yake, amewaonya kuwa dawa yao ipo
jikoni.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, Lulu
alisema kuwa kila kukicha lazima watu hao waibuke na jipya linalomhusu
yeye, mbaya zaidi ni kwa ajili ya kumchafua.
“Mara utasikia Lulu kagombania bwana, mara Lulu kafanya sijui kitu
gani lakini ukiangalia hakuna hata cha ukweli kwa kuwa nimekuwa staa
basi kila mtu ana lake la kuongea, kifupi nimeshawajua wabaya wangu na
kwamba ni wengi sana, nawaambia niko njiani kuwaandalia dawa yao ambayo
naamini itakuja kuwa fundisho kwao na kwa wengine,” alisema Lulu.
Hii ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kufunguka kuhusu suala hilo
lakini Ijumaa Wikienda linamuomba asichukue sheria mkononi kwani kibao
kinaweza kumgeukia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment