MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU ABAKWA NA KUNAJISIWA NA MWANAUME WA MIAKA 30 HUKO ARUSHA
Na.Joseph Ngilisho,Arusha
Ukistajabu ya Mussa, utapata ya Firauni,mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu (jina linahifadhiwa),mkazi wa Sokoni One jijini hapa, amebakwa na kunajisiwa na mwanamme mwenye umri wa miaka 30. Mtuhumiwa ametajwa kwa jina la Rajabu Mkoba, mkazi wa eneo hilo.
Ilidaiwa mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo kwa zaidi ya saa 9 baada ya kumchukua kwa mtu aliepewa kumtunza. Tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu huku mama mzazi wa mtoto huyo, Mwitango Yambazi Mtalu (27), akishindwa kutoa taarifa polisi baada ya kuahidiwa shilingi 100,000.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mama wa mtoto huyo, alisema siku ya Jumapili majira ya asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga, ili apate nafasi ya kushiriki mkutano wa kikundi chake.
Alisema baada ya kurudi jioni majira ya saa mbili usiku alikwenda kwa jirani yake huyo kwa lengo la kumchukua mtoto wake lakini aliarifiwa mtoto wake alichukuliwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Rajabu ambaye anafahamika eneo hilo.
Alisema aliamua kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ambaye anaishi na wazazi wake, hata hivyo hakufanikiwa kumkuta wala mtoto wake na kurejea nyumbani huku akiendelea na jitihada za kumtafuta.
Alisema aliamua kwenda kituo cha polisi Unga Limited kumuulizia akiongozana na balozi wa nyumba kumi.
Hata hivyo, polisi walimtaka arudi nyumbani hadi asubuhi arejee kituloni kwa ajili ya taratibu nyengine.
Alisema wakati akirejea nyumbani majira ya saa 9 usiku alimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa aliyetambukika kwa jina la mama Mkoba akiwa na mtoto wake akimrejesha huku mtuhumiwa akiwa hayupo.
Baada ya kukabidhiwa aliamua kumchunguza vizuri ndipo alipokuta sehemu za siri za mtoto wake zimevimba kupita kiasi huku damu ikitoka mara kwa mara.
Aliamua kumweleza mama wa mtuhumniwa jinsi mtoto wake alivyoharibiwa, ambapo mama huyo alimsihi asitoe taarifa popote na kwamba atampatia shilingi 100,000 na kumpeleka mtoto huyo hospitali.
Hata hivyo, mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo, hakumpeleka hospitali yeyote badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.
Lakini baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mama wa mtoto kunyamazia unyama huo ndipo walipomvamia kwa maneno makali na kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kwenda kituo cha polisi Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kumpeka hospitali ya Mount Meru.
Mama wa mtoto huyo na wa mtuhumiwa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano huku mtuhumiwa akiendelea kusakwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment