Mapenzi
ya Kibongo ni ya aina yake duniani, hivyo nimeona leo nitoe somo ili
kuwasaidia mayanki namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongo.
Kwanza mapenzi ya Kibongo hayashughuliki na mambo madogomadogo kama eti
kupeana maua au eti kutembea beach mmeshikana mikono, hizo ishu ni za
kwenye sinema tu au labda Ulaya.
Hapa watu wako bize wanahangaika na maisha, mambo hayo ni ya wazungu.
Wapenzi wa Kibongo wa ukweli huwa hawahangaiki kuelezana eti I love you
au nakupenda sana, aaa wapi, mdada akiwa na mapenzi ya ukweli utaona
anampikia mpenzi wake chakula cha ukweli.
Jamaa anapokula msosi anajua kuwa kweli huyu mdada ananipenda, hapo
hata kama amewakaribisha mabest zake, utasikia ‘Aise huyu demu
anakupenda sana kakupikia chakula kitamu hivi’.
Katika mapenzi ya Kibongo bili zote mwanaume lazima ulipe.
Mkiwa mmekaa baa mmeshakula na kunywa sana hata kama mwanaume unaona
mdada kaanza kushika pochi kama vile anataka kulipa jua ni geresha tu,
anajua unampenda hivyo utalipa tu.
Hata wale wadada waliowahi kuishi Ulaya wanajua ‘system’ ya Bongo ni
mwanaume kulipa. Katika mapenzi ya ukweli ya Kibongo, mdada hata amkute
bwana wake na binti mwingine, hata kama wamekaa kihasara ili kuonyesha
mapenzi ni muhimu kumezea, tena unafanya kama hujaona chochote!
Hii itamfanya jamaa ajue unampenda sana, japokuwa mapenzi ya Kibongo
yana mipaka, mdada haruhusiwi kukutwa amekaa kihasara na mkaka. Ili
mwanaume wa Kibongo aonyeshe anampenda sana mpenzi wake, wivu huwa
muhimu, mwanaume yeyote, hata kama ndugu marufuku kumsalimia au kutuma
meseji au kuchat kwenye simu, hasa giza likianza kuingia.
Jambo lingine muhimu katika mapenzi ya Kibongo, mwanaume wa Kibongo
marufuku jikoni, kwa sababu mdada anakupenda hata ukirudi saa kumi za
usiku na ukamkuta ana malaria kali, lazima ajikongoje aingie jikoni,
mwanaume ukikosea tu uanze kuingia jikoni kupika ujue umeanzisha mtindo
utakaokukosti akipona atadai uendelee kupika na kuosha vyombo na
kadhalika. Chunga sana!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment