MWIGIZAJI nyota wa filamu, Rose Ndauka ameibuka na
kukanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa uchumba wake na Malick Bandawe
umevunjika na kusema siyo kweli kwani bado upo ngangari kuliko kawaida.
Akistorisha na gazeti hili juzikati, mwigizaji huyo anayeishi na
mchumba wake huyo, alisema uvumi huo hauna msingi kwa sababu asubuhi ya
siku hiyo (Jumatatu) alikuwa amemnyooshea nguo alizovaa wakati akielekea
kazini kwake.
Awali, kulikuwa na madai ya kuwepo kwa mtafaruku baina ya wawili hao
na kudaiwa kuachana kutokana na mmojawapo kulala nje siku tatu, kitendo
kilichochochewa na kuonekana kwa Rose akiwa peke yake wakati wa fainali
za kumtafuta msanii chipukizi zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani
City wiki iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment